Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Sir Ferguson aingia matatani tena na Chama Cha Soka Uingereza FA

Kocha wa Manchester United “Mashetani Wekundu” Sir Alex Ferguson ameingia matatani kwa mara nyingine kwa utovu wa nidhamu na huenda Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kikampa adhabu kutokana na maneno yake aliyoyatoa dhidi ya Mwamuzi Howard Webb.

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akilalama kwenye moja ya michezo ya klabu yake
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akilalama kwenye moja ya michezo ya klabu yake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ferguson ameingia matatani kwa mara nyingine baada ya kutoa maneno ya kumsifia Webb kuwa ni Mwamuzi bora ambaye anajua kazi yake kabla ya mchezo wao dhidi ya Chelsea ambao walishinda kwa magoli 2-1.

FA kwenye taarifa yake imesema Ferguson amekiuka kanuni kutokana na kumuongelea mwamuzi kabla ya mchezo kitu ambacho kinaweza kikamfanya akapewa adhabu.

Ferguson ambaye ameshuhudiwa akipewa adhabu ya kutokuwepo kwenye benchi kwa michezo mitano ya Ligi baada ya kumkosoa vikali Martin Atkinson ambaye alichezesha mchezo wa kwanza dhidi ya Chelsea huku Manchester wakipata kichapo cha magoli 2-1.

Kocha huyo wa Mashetani Wekundu alimsifia Mwamuzi Webb ambaye alichezesha mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia na kusema hakuna mwenye mashaka juu ya kazi yake.

Ferguson kabla ya mchezo alinukuliwa akisema Mwamuzi ambaye amepangwa ni mzuri kwa hiyo ni jukumu lako kuhakikisha wanafanikiwa kukaribia ubingwa kwa kushinda mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Kocha huyo amepewa muda hadi tarehe 16 ya mwezi May kuweza kujibu tuhuma ambazo zinamkabili za utovu wa nidhamu kabla ya kuanza kutekelezwa kwa adhabu hiyo.

Ferguson kocha mkongwe kwa sasa anasaka rekodi ya kuipa taji la 19 Manchester United ambayo itakuwa na kibarua dhidi ya Blackburn Rovers huku wakitakiwa kupata pointi moja pekee kabla ya kutwaa ubingwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.