Pata taarifa kuu

Mazungumzo kati ya Hamas na Israeli yamevunjika

Nairobi – Ujumbe wa kundi la Hamas umeondoka jijini Cairo, baada ya mazungumzo na wasuluhishi wa mzozo wake na Israeli kuvunjika, kufuatia jitihada za siku kadhaa za kujaribu kupata mkataba  wa kusitisha vita kabla ya kuanza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wapatanishi wamekuwa wakitaka kupatikana kwa muafaka kati ya Israeli na Hamas kabla ya mwezi wa Ramadhan
Wapatanishi wamekuwa wakitaka kupatikana kwa muafaka kati ya Israeli na Hamas kabla ya mwezi wa Ramadhan © Ammar Awad / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa juu wa Hamas, amesema wanakwenda jijini Doha kwa mashauriano zaidi, huku akiilaumu Israeli kwa kukwamisha harakati za kupata makubaliano ya kusitisha vita.

Aidha, amesema wanasbiri majibu ya Israeli kuhusu namna ya kukubaliana baada ya kutoridhishwa namna mpinzani wake, anavyotaka vita hivyo kusitishwa.

Ripoti zinasema kuwa, Israeli inataka Hamas kutoa orodha ya mateka wote walio hai, lakini kundi hilo linasema hatua hiyo itawezekana tu baada ya mkataba wa kusitisha vita kupatikana.

Marekani, Misri na Qatar zimekuwa zikiongoza mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kati ya Hamas na Israeli
Marekani, Misri na Qatar zimekuwa zikiongoza mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kati ya Hamas na Israeli © Amir Cohen / Reuters

Marais wa Marekani Joe Biden, ambaye ametuma wajumbe wake kusaidia kupata suluhu, wiki hii alitoa wito kwa Hamas kukubali mpango wa kumaliza vita na Israeli kabla ya mwishoni mwa wiki hii, kabla ya kuanza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo, matumaini ya kupata mkataba huo, yamedidimia wakati huu jeshi la Israeli linapoendelea kushambulia Gaza kwa mwezi wa sita sasa, na usiku wa kuamkia leo, watu wengine 83 waliuawa na kufikisha idadi ya Wapalestina walipoteza maisha hasa wanawake na watoto kufikia 30,800.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Niger, Mali na Burkina Faso zimetangaza kuunda jeshi la pamoja, kupambana na makundi ya kijihadi katika nchi zao.

 

Mkuu wa Majeshi wa Niger, Moussa Salaou Barmou ametangaza muungano huo, ambaye amesema, operesheni ya jeshi hilo la pamoja, itaanza hivi karibuni.

 

Hata hivyo, hajaeleza kikosi cha jeshi hilo linaundwa na wanajeshi wangapi.

 

Hatua hii inakuja baada ya mwezi Septemba mwaka uliopita, nchi hizo ambazo pia zilitangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya ECOWAS, zilitangaza muungano mpya wa kijeshi baada ya kujiondoa kwenye kikosi cha Kimataifa cha G5.

 

Hali ya usalama katika nchi hizo tatu, imeendelea kuwa mbaya kwa muda wa miaka 10 kutokana na uwepo wa makundi ya kijihadi na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, koloni ya zamani ya nchi hizo tatu, imesababisha hali kuendelea kuwa mbaya.

 

Jeshi hilo la pamoja, pia linatarajiwa kuchukua nafasi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MINUSMA, ambacho mwezi Desemba mwaka uliopita, liliondoka kwenye nchi hizo baada ya kufukuzwa na viongozi wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.