Pata taarifa kuu

Philippe Lazzarini: Israel inataka kuangamiza UNRWA

Israel inaendesha kampeni ya pamoja inayolenga kuangamiza UNRWA, mkuu wa shirika hili la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina amesema katika mahojiano yaliyochapishwa Jumamosi.

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, Desemba 6, 2023.
Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, Desemba 6, 2023. AP - Bilal Hussein
Matangazo ya kibiashara

 

Philippe Lazzarini alizingatia haswa kwamba ombi la Israeli llinalotaka ajiuzulu lilikuwa sehemu ya kampeni hii. "Kwa sasa tunakabiliwa na kampeni kubwa na ya pamoja ya Israel inayolenga kuangamiza UNRWA," ameliambia kundi la magazeti la Uswisi la Tamedia.

"Hili ni lengo la muda mrefu la kisiasa, kwa sababu wanaamini kwamba ikiwa shirika hilo litafutwa, suala la hadhi ya wakimbizi wa Kipalestina litatatuliwa mara moja na kwa wote, na pamoja na shirika hilo, haki ya kurejea itazingatiwa.

Kuna lengo pana zaidi la kisiasa nyuma ya hali hii, "ameongeza. UNRWA iliundwa mnamo 1949 kuhudumiwa wakimbizi wa Kipalestina kufuatia vita vya kwanza vya Waarabu na Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.