Pata taarifa kuu

Gaza: UNRWA yawafuta kazi wafanyakazi wanaotuhumiwa kuhusishwa na mashambulizi ya Hamas

Kufukuzwa kazi mara moja na uchunguzi wa wazi: mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) mara moja alichukua maamuzi haya baada ya kujua kwamba Israel inawatuhumu wafanyakazi wake kadhaa kushiriki katika mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7.

Wananchi wa Gaza wakipokea mifuko ya unga inayotolewa na UNRWA huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 21, 2023.
Wananchi wa Gaza wakipokea mifuko ya unga inayotolewa na UNRWA huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 21, 2023. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), linaloshtumiwa na mamlaka ya Israel kwa muda mrefu, limetangaza siku ya Ijumaa, Januari 26, kwamba limejitenga na wafanyakazi kadhaa, wanaotuhumiwa kuhusishwa na mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7. "Mamlaka ya Israel imeipatia UNRWA taarifa kuhusu kuhusika kwa wafanyakazi wake kadhaa" katika shambulio hilo, inabainisha taarifa kutoka kwa mkuu wa shirika hilo, Philippe Lazzarini, bila kutaja idadi yao kamili au utambulisho wao.

UNRWA ni shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linajishughulisha na kusambaza misaada kwa raia katika Ukanda wa Gaza, na kwa hiyo linakabiliwa na hali nzito kutokana na mapigano ya ardhini katika eneo hilo. "Ili kulinda uwezo wa shirika hili la Umoja wa Mataifa kwa kutoa misaada ya kibinadamu, nimeamua kusitisha mara moja kandarasi za wafanyakazi hawa na kufungua uchunguzi," ameongeza Philippe Lazzarini. “Mtumishi yeyote ambaye amejihusisha na vitendo vya ugaidi atawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria. "

Wakati huo huo, shirika hilo limekariri "kulaani kwake kwa maneno makali" ya shambulio la Oktoba 7 na linataka kuachiliwa "mara moja na bila masharti" kwa mateka wa Israeli ambao bado wanazuiliwa. Hata hivyo, linasisitiza juu ya ukweli kwamba "zaidi ya watu milioni 2 huko Gaza wanategemea misaada muhimu ambayo shirika hilo limetoa tangu vita vilipoanza" na kwamba "mtu yeyote anayesaliti maadili ya msingi ya Umoja wa Mataifa pia anawasaliti wale tunaohudumia Gaza, katika ukanda na kwingineko duniani.”

Washington inasitisha "kwa muda"  ufadhili wake

Dakika chache baadaye, Washington imetoa jibu kali, ikitangaza kwamba "itasitisha" kwa muda ufadhili wowote wa ziada kwa shirika la Umoja wa Mataifa, wakati linachunguza madai haya. "Marekani inasikitishwa sana na shutuma kwamba wafanyakazi kumi na wawili wa UNRWA huenda walihusika katika shambulio la kigaidi la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller, katika taarifa.

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken amezungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ili "kusisitiza haja ya uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu suala hili". Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, kwa upande wake, pia inadai "uchunguzi wa ndani wa shughuli za Hamas na mashirika mengine ya kigaidi" ndani ya UNRWA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.