Pata taarifa kuu

Victor Osimhen achaguliwa mchezaji bora wa Afrika wa mwaka

Mshambulizi wa Nigeria Victor Osimhen, 24, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika wa mwaka wa 2023 siku ya Jumatatu, wakati wa hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika huko Marrakech, Morocco.

Mnigeria Victor Osimhen ametwaa Taji la Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka 2023.
Mnigeria Victor Osimhen ametwaa Taji la Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka 2023. AP - Massimo Paolone/
Matangazo ya kibiashara

Osimhen, bingwa wa Italia na Naples msimu uliopita na mshindi wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopita, alikuwa akiwania tuzo hii na Mmisri Mohamed Salah (Liverpool) na beki wa Morocco Achraf Hakimi (Paris SG).

Nahodha wa Misri, Salah alishinda tuzo ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mwaka 2017 na 2018 - na alishika nafasi ya pili kwa Sadio Mane 2019 na 2022 - wakati beki wa kulia Hakimi alikuwa na jukumu muhimu katika kampeini ya kihistoria ya Morocco hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia la Fifa 2022.

Hata hivyo Osimhen alikuwa mchezaji wa daraja la juu zaidi wa Kiafrika katika kura ya Ballon d'Or kwa upande wa Wanaume 2023, akimaliza wa nane baada ya kufunga mabao 26 msimu uliopita na kuisaidia Napoli kutwaa taji lao la kwanza la Serie A ndani ya miaka 33.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.