Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Mlipuko wapiga Taba, mji wa Misri unaopakana na Israel

Mlipuko ulitokea usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa Oktoba 27 katika mji wa Taba nchini Misri, kwenye mpaka na bandari ya Israel ya Eilat kwenye Ghuba ya Akaba katika Bahari Nyekundu. Watu sita wamejeruhiwa kidogo na uchunguzi umefunguliwa.

Bendera za Israeli, kushoto, na bendera za Misri kwenye nguzo ya mpaka kati ya nchi hizo mbili huko Taba.
Bendera za Israeli, kushoto, na bendera za Misri kwenye nguzo ya mpaka kati ya nchi hizo mbili huko Taba. AP - ENRIC MARTI
Matangazo ya kibiashara

Habari ya kwanza ilizungumzia kuhusu kombora, au roketi, iliyoanguka karibu saa nane usiku huko Taba, mji ulio kwenye Bahari Nyekundu, ulio kwenye ncha ya kaskazini-mashariki ya Sinai na ambako kuna nguzo ya mpaka kuelekea Israeli. Kombora lililoanguka usiku hatimaye lilikuwa ndege isiyo na rubani yenye asili isiyojulikana, amesema msemaji wa jeshi la Misri.

Mlipuko huo uliharibu jengo ambalo timu za madaktari wa hospitali hiyo katika mji mdogo wa pwani huishi, anaripoti mwandishi wetu wa Cairo, Alexandre Buccianti. Watu sita wamejeruhiwa kidogo. Tangu wakati huo wameruhusiwa kutoka hospitali. Picha zinazorushwa kwenye vyombo vya habari vya ndani au mitandao ya kijamii zinaonyesha jengo lililoharibiwa na magari kadhaa yamelipuliwa katika eneo jirani.

Mapema leo Ijumaaasubuhi, bandari ya Nuweiba, iliyoko kilomita 70 zaidi kusini, ilikumbwa na mlipuko mdogo ambao haukusababisha majeruhi.

Kuelekea jibu la Misri?

Vyombo vya habari vya Misri vinaongelea kuwa ndege hiyo ilirushwa kimakosa au uchochezi wa Israeli. Msemaji wa jeshi la Misri amebaini kwamba uwezekano kwamba mji wa Eilat ndio ulikuwa umelengwa haujatengwa na wachunguzi.

Mamlaka ya Misri imebaini kwamba zinahifadhi haki ya kulipiza kisasi dhidi ya yeyote aliyehusika na milipuko hii. Taba, maarufu kwa watalii wa Israeli, ilikumbwa na mashambulizi ya umwagaji damu ya wanamgambo wa Kiislamu mnamo mwaka 2004 na 2014.

Rasi ya jangwa la Sinai imepakana na ncha yake ya kaskazini-magharibi na Ukanda wa Gaza na inashiriki mpaka wake wa mashariki na Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.