Pata taarifa kuu

Israel yaghadhabishwa na Moscow kwa kupokea ujumbe wa Hamas

Ujumbe wa Hamas uko Moscow kwa ziara rasmi ya majadiliano kuhusu vita vinavyoendelea kwa wiki tatu, diplomasia ya Urusi ilibainisha siku ya Alhamisi, Oktoba 26. Ujumbe wa Hamas unaongozwa na Musa Abu Marzouk, naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya kundi hilo. Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov alikutana na viongozi wa kisiasa wa Hamas nchini Qatar, kulingana na vyombo vya habari vya Urusi. hali inayoifanya Israeli kupandwa na hasira.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov alikutana na viongozi wa kisiasa wa Hamas nchini Qatar, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi.Hali ambayo inaifanya Israeli kupandwa na hasira.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov alikutana na viongozi wa kisiasa wa Hamas nchini Qatar, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi.Hali ambayo inaifanya Israeli kupandwa na hasira. AP - Natalia Kolesnikova
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Israel inashutumu vikali mazungumzo haya na Hamas, na hasa mapokezi ya ujumbe wa kundi hilo la Palestina mjini Moscow. Hamas, inasisitiza Wizara ya Mambo ya Nje huko Jerusalem, ni "shirika la kigaidi baya kuliko Daesh (kundi la Islamic State)".

"Mikono ya maofisa wake wakuu imefunikwa na damu ya Waisraeli zaidi ya 1,400 ambao waliuawa kinyama, waliangamizwa, waliuawa na kuchomwa moto," imeongeza serikali ya Israel. "Wanawajibika pia kwa utekaji nyara wa Waisraeli zaidi ya 220, ikiwanipamoja na watoto wachanga, watoto na wazee", inakumbuka diplomasia ya Israeli katika ujumbe uliotumwa kwa Kremlin.

Kwa mujibu wa Israeli, mwaliko wa Moscow kwa ujumbe huu ni "tendo chafu la kuunga mkono ugaidi na uhalalishaji wa Hamas". Wizara ya Israel inatoa wito kwa serikali ya Urusi kuwafukuza mara moja "magaidi wa Hamas".

Hata hivyo mamlaka ya Urusi halichukulii kundi la Hamas kuwa la kigaidi.

Tangu kuanza kwa vita hivyo, kumekuwa na mazungumzo ya simu kati ya Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Rais wa Urusi alikuwa amewasilisha rambirambi zake kwa Israeli, lakini tangu wakati huo, nchi yake "imejipanga kwa utaratibu pamoja na Hamas", Israel imesema katika taarifa. Na inaelezwa kuwa, ikiwa tangu kuanza kwa mzozo na Ukraine, Israel imekuwa kimya katika ukosoaji wake kwa Urusi, sasa mambo yamebadilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.