Pata taarifa kuu

Wawakilishi wa Hamas na Iran mjini Moscow kwa mazungumzo

Wiki tatu baada ya kuanza kwa mzozo wa Hamas na Israel, ujumbe kutoka kundi la wanamgamo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina ulikuwa mjini Moscow Alhamisi hii, Oktoba 26. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani pia alikuwa katika mji mkuu wa Urusi. Taarifa juu ya ajenda na yaliyozungumzwa imesalia kuwa siri.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amekutana mjini Moscow na mwenzake wa Urusi Mikhail Bogdanov mnamo Oktoba 26, 2023. Wawili hao wamejadili kuhusu "kuongezeka kwa mapigano katika mzozo wa Israel na Palestina," kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amekutana mjini Moscow na mwenzake wa Urusi Mikhail Bogdanov mnamo Oktoba 26, 2023. Wawili hao wamejadili kuhusu "kuongezeka kwa mapigano katika mzozo wa Israel na Palestina," kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. AP - Vahid Salemi
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Mawasiliano rasmi ya Urusi yamesalia kuwa siri. Ni baadhi tu ya mistari michache iliyowekwa wazi mwishoni mwa siku kwenye tovuti ya Waziri wa Mambo ya Nje: "ajenda ya kikanda imejadiliwa kwa kina, na msisitizo umewekwa kwenye kuongezeka kwa kasi kwa mapigano ambayo haijawahi kushuhudiwa katika eneo la migogoro la Palestina na Israel. Wakati huo huo, haja ya kusitisha mapigano ndani na nje ya Ukanda wa Gaza na kutoa msaada wa haraka wa kibinadamu kwa wakazi wa Palestina walioathirika imesisitizwa.

Mapema mchana, ufafanuzi huu madhubuti pekee ulitolewa kupitia mashirika ya habari ya Urusi: majadiliano yamelenga mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas kutoka Palestina.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Ikulu ya Kremlin kwa Mashariki ya Kati, alikuwa tayari ameonya wiki mbili zilizopita: "Hatua hii inahitaji diplomasia ya busara badala ya matamko yenye lengo la kuchochea uhasama."

Kwa siku kadhaa, nchini Urusi, vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kushindwa kwa serikali kutoa matamshi makali dhidi ya Hamas, kundi ambalo mamlaka ya Urusi halichukulii kuwa la kigaidi.

Akihojiwa Jumanne hii juu ya swali la mateka wa Hamas, msemaji wa Kremlin alitoa wito wa kuachiliwa mara moja bila kutofautisha utaifa. "Huu ndio msimamo wetu thabiti," alisema Dmitri Peskov.

Haijulikani ni lini wawakilishi wa Hamas wataondoka Moscow, lakini Kremlin imeonya: "Vladimir Putin hana nia ya kukutana na ujumbe wa Hamas uliopo Moscow. Lakini ziara ya kiongozi wa mamlaka ya Palestina Abbas inatarajiwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.