Pata taarifa kuu

Tetemeko la ardhi Uturuki na Syria: Marekani kuipa msaada Uturuki na Syria

Marekani imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 85 kwa Uturuki na Syria baada ya tetemeko la ardhi kuua watu zaidi ya 28,000 na kujeruhi zaidi ya 75,000 na kuwaacha milioni tano bila makazi. Maelfu ya masanduku yaliyojaa michango yanawasili katika ubalozi wa Washington na watu wanaoishi nje ya nchi waliotawanyika kote Marekani wanashiriki katika msaada huu.

Huko Adiyaman, familia zinazika wapendwa wao, wahanga wa tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki na Syria wiki moja iliyopita.
Huko Adiyaman, familia zinazika wapendwa wao, wahanga wa tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki na Syria wiki moja iliyopita. AP - Emrah Gurel
Matangazo ya kibiashara

Msaada hiyo ni pamoja na mifuko ya kulalia, blanketi, mahema, nepi zilizotolewa na wakaazi wa Texas. Lamah ana asili ya Kipalestina anasema : “Zoezi linakwenda vizuri. Sisi ni familia moja katika Mashariki ya Kati, na ninahisi hitaji la kusaidia kadiri niwezavyo. "

Mkuu wa kitengo cha misaada cha Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema hadi sasa imeshindikana kuwafikia watu wa kaskazini-magharibi mwa Syria. Ameeleza msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba vifaa kuelekea kaskazini magharibi mwa Syria umewasili kupitia Uturuki kwa ajili ya mamilioni ya watu ambao nyumba zao ziliharibiwa na mitetemeko iliyotokea lakini imechelewa kufika Syria.

Syria kwa miaka mingi inakabiliwa na migogoro hali ambyo imesababisha kuzorota kwa utoaji wa huduma za afya huku baadhi ya sehemu katika nchi hiyo zinaendelea kudhibitiwa na  waasi wanaopambana na serikali ya Rais Bashar al-Assad, ambayo imewekewa vikwazo nan chi za Magharibi.

Wakati huo huo maelfu ya waokoaji wanaendelea kuvifikia vitongoji vilivyoharibiwa na mitetemeko hiyo wakati ambapo baridi kali inaongeza huzuni kwa mamilioni ya watu wanaohitaji msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.