Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Antony Blinken azuru Cairo kabla ya kuelekea Jerusalem na Ramallah

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili Jumapili hii Januari 29 mjini Cairo, nchini Misri. Misri ni hatua ya kwanza ya ziara ya mkuu wa diplomasia ya Marekani katika Mashariki ya Kati, ziara ambayo inapaswa kumpeleka Jumatatu hii nchini Israel na Jumanne kwenda Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atembelea Chuo Kikuu cha Marekani mjini Cairo, Misri, Jumapili, Januari 29, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atembelea Chuo Kikuu cha Marekani mjini Cairo, Misri, Jumapili, Januari 29, 2023. AP - Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ilikuwa imepangwa kwa muda mrefu, lakini kuzuka kwa ghasia za ghafla kati ya Waisraeli na Wapalestina kunaipa umuhimu mpya kabisa.

Shambulio la Alhamisi kwenye kambi ya wakimbizi huko Jenin, Ukingo wa Magharibi, na kusababisha vifo vya watu tisa, na mashambulio mawili ya vijana wa Kipalestina, moja karibu na sinagogi huko Jerusalem Mashariki na kuua saba, lingine huko Silwan, umbali wa kutupa jiwe kutoka Mji Mkongwe lilisababisha watu wawaili kujeruhiwa, hakika yatakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Je, Antony Blinken atafanikiwa kutuliza mambo? Kupunguza mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina? Na ni wakati Waziri Mkuu mpya Benjamin Netanyahu anaongoza serikali ya kitaifa zaidi katika historia ya Israel na kuahidi kuchukua msimamo mkali juu ya Wapalestina? Na kwamba kiongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas, mwenye umri wa miaka 87 na asiyependwa, ana ushawishi mdogo sana kwa vijana wenye hasira?

Antony Blinken ataomba hitaji la "kuchukua hatua za haraka za kupunguza" mvutano, amebainisha msemaji wa wizara ya mabo ya nje ya Marekani. Mjini Cairo, mkuu wa diplomasia ya Marekani atajaribu kumshawishi rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, kwa mara nyingine kuchukua nafasi ya mpatanishi na Wapalestina.

Mjini Jerusalem siku ya Jumatatu na mjini Ramallah siku ya Jumanne, Bw. Blinken anatarajiwa kuunga mkono Marekani kwa suluhu la mataifa mawili ya Israel na Palestina.

Kifo cha Mpalestina mwenye umri wa miaka 18, aliyeuawa na walinzi wa Israel karibu na makazi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, hakitafanya kazi yake kuwa rahisi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.