Pata taarifa kuu

UN imetuhumu uwongozi wa Lebanon kwa changamoto zinazowakumba raia wake.

Umoja wa mataifa UN, umeituhumu serikali ya Lebanon na benki kuu kwa mgogoro wa kifedha unaoshuhudiwa katika taifa hilo, mzozo ambao umechangia katika ongezeko la idadi ya watu wanaoishi kwa umaskini kwenye taifa hilo.

Raia wa Lebanon wakipiga foleni nje ya duka la kubadilisha pesa.
Raia wa Lebanon wakipiga foleni nje ya duka la kubadilisha pesa. © REUTERS - MOHAMED AZAKIR
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya mjumbe maalum wa UN, Olivier De Schutter, kuhusu hali ya umaskini na viwango vya haki za binadamu imeeleza kuwa mgogoro huo wa kifedha ulisababishwa na uwepo wa sera mbovu kutoka kwa serikali ya Lebanon yenyewe.

UN, aidha imetoa wito kwa mamlaka nchini Lebanon kubadili mwelekeo kuelekea uchaguzi wa wabunge ambao umeratibiwa kufanyika mei 15.

Tangu mwaka mwa 2019 sarafu ya Lebanon imepoteza zaidi ya asilimia 90 ya thamani yake dhidi ya dolla, bei za bidhaa zikitajwa kupanda kwa zaidi ya asilimia 200, viwango vya umaskini vikipanda kwa asilimia 80 ya idadi ya raia nchini humo.

Iwapo kutakuwepo na uwazi na uwajibikaji kwa viongozi nchini humo huenda hali ngumu ambao raia wanapatia ikabadilika imesisitiza ripoti hiyo.

Olivier De Schutter, mjumbe maalum wa UN, alifanya ziara jijini Beirut mwaka wa 2021 mwezi Novemba kutathimini athari za mzozo wa kifedha kwa maisha ya raia wa kawaida pamoja na uchumi wa Lebanon.

Watu sita kati ya kumi nchini humo  humo wameonyesha nia ya kuondoka kwenye taifa hilo iwapo watapewa nafasi ya kwenda kutafuta maisha mazuri kwengine, watu tisa kati ya kumi wakiwa wanapitia wakati mgumu kujikimu kimaisha hali ambayo UN inasema ingeepukika.

Lebanon inajiaanda kuwa ajili ya uchaguzi wa wabunge mei 15, uchaguzi mwa kwanza kufanyika tangu taifa hilo kutumbukia katika mzozo huo wa kifedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.