Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Msikiti mmoja nchini Afghanistan washambuliwa

Bomu limelipuka katika msikiti mmoja wakati wa sala ya Ijumaa, na kujeruhi watu 15 mashariki mwa Afghanistan, ambapo wanamgambo wa ISIS wanaendesha kampeni ya machafuko.

Bomu lililolipuka katika msikiti mmoja wakati wa sala ya Ijumaa,limejeruhi watu 15 mashariki mwa Afghanistan.
Bomu lililolipuka katika msikiti mmoja wakati wa sala ya Ijumaa,limejeruhi watu 15 mashariki mwa Afghanistan. © ILNA
Matangazo ya kibiashara

Qari Hanif, msemaji wa serikali ya jimbo la Nangarhar, alisema bomu hilo linaonekana kuwa liliwekwa ndani ya msikiti huo katika mji wa Traili, ulioko katika eneo la milima la Spin Ghar, nje ya mji mkuu wa jimbo hilo Jalalabad.

Tangu kuchukua madaraka nchini Afghanistan miezi mitatu iliyopita, kundi la Taliban limeendesha kampeni ya kukabiliana na waasi, wakiapa kukomesha tishio la ISIS.

Makundi yote mawili yana msimamo mkali wa dini ya Kiislamu na kwa miaka mingi yamejihusisha na baadhi ya mbinu zilezile za vurugu, kama vile mashambulizi ya kujitoa mhanga. Hata hivyo, kundi la Taliban limelenga kuchukua udhibiti wa Afghanistan, huku Dola la Kiislamu likizingatia jihad ya kimataifa.

Msemaji wa idara ya kijasusi ya Taliban aliwaambia waandishi wa habari mjini Kabul siku ya Jumatano kwamba idara hiyo limewakamata karibu wapoganaji 600 wa ISIS, wakiwemo watu muhimu na wafadhili wa kifedha. Msemaji wa idara ya ujasusi, Khalil Hamraz, alisema takriban wanaharakati 33 wa ISIS waliuawa katika mapigano na vikosi vya usalama vya Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.