Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Afisa wa Taliban auawa katika mashambulizi dhidi ya hospitali Kabul

Mkurugenzi wa vikosi vya jeshi vya Taliban huko Kabul, Hamdullah Mokhlis, ni miongoni mwa waathirika wa shambulio la Jumanne, Novemba 2 lililotekelezwa na kundi la Islamic State dhidi ya Hospitali ya Jeshi la Mji wa Afghanistan, kulingana an achanzo cha serikali.

Watu wasiopungua 19 wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya hospitali ya kijeshi mjini Kabul jana Jumanne.
Watu wasiopungua 19 wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya hospitali ya kijeshi mjini Kabul jana Jumanne. AFP - HOSHANG HASHIMI
Matangazo ya kibiashara

Kamanda Mokhlis mmoja wa viongozi wa kundi la Haqani, anayetuhumuwa gaidi na Marekani, ni kiongozi wa ngazi ya juu wa Taliban aliyeuawa tangu Taliban kuchukuwa madaraka nchini Afghanistan, katikati ya mwezi wa Agosti.

Watu wasiopungua 19 wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya hospitali ya kijeshi mjini Kabul jana Jumanne. Kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo la risasi na bomu katikakati mwa mji mkuu.

Kundi hilo lilisema katika taarifa kwenye chaneli yake ya Telegram kuwa wapiganaji watano wa Dola la Kiislamu walifanya mashambulizi yaliyoratibiwa kwa wakati mmoja.

Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema waasi hao wa IS walitaka kuwalenga raia, madaktari na wagonjwa hospitalini hapo, na kuongeza kuwa vikosi vya Taliban vilizima shambulizi hilo katika muda wa dakika 15. Taliban ilitumia miaka 20 ikiendesha uasi dhidi ya serikali iliyokuwa inaungwa mkono na Marekani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.