Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI

Marekani yalaani kauli ya Erdogan juu ya Wayahudi wanaochukuliwa kuwa "wabaguzi"

Marekani imeichukulia kauli ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kama ya kichochezi kuhusiana na Wayahudi, ambao aliwaita hivi karibuni kuwa ni wabaguzi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Novemba 7, 2019.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Novemba 7, 2019. REUTERS - BERNADETT SZABO
Matangazo ya kibiashara

"Tunamsihi Rais Erdogan na viongozi wengine wa Uturuki kujiepusha na matamshi yoyote ya uchochezi, ambayo yanaweza kuchochea ghasia zaidi," Ned Price amesema katika taarifa.

"Maneno ya kibaguzi hayana nafasi popote," ameongeza.

Ned Price hakusema kauli gani Recep Tayyip Erdogan aalitoa mabyo Marekani inaichukulia kama ya kichochezi.

Recep Tayyip Erdogan, ambaye anatetea vikali Wapalestina, alikosoa Israeli kwa mashambulio yake ya anga huko Gaza na kuiita israel kama "taifa la kigaidi" baada ya polisi wa Israeli kufyatua risasi za mpira kwa Wapalestina wakirusha mawe huko Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.