Israeli yafuta sharti la uvaaji barakoa
Israeli imechukua uamuzi wa kufuta sharti la watu kuvaa barakoa wakiwa nje ya makwao na kufungua shule zote, hatua ya mwisho kuelekea kurudi kwa maisha ya kawaida kutokana na kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya janga la orona iliyofanywa nchini
Imechapishwa:
Israeli imeshuhudiwa kupungua kwa kasi kwa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, na karibu 54% ya idadi ya watu milioni 9.3 wamechomwa sindano mbili za chanjo ya Pfizer / BioNTech.
Sharti la kuvaa barakoa, hatua iliyokuwa chini ya idara ya polisi na kuamriwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, limefutwa Jumapili hii, lakini wizara ya afya imeeleza kwamba bado shati hili linahitajika katika nafasi za umma za ndani, ikiwataka raia kila wakati kuwa na barakoa karibu.