Pata taarifa kuu
PALESTINA

Makundi hasimu nchini Palestina yakubaliana juu ya utaratibu wa uchaguzi

Uchaguzi nchini Palestina uliopangwa kufanyika mwaka huu utaendelea kama ilivyopangwa na matokeo yake yataheshimishwa, makundi hasimu ya Wapalestina yamesema katika taarifa ya pamoja.

Mmoja ya raia wa Palestina katika moja ya maandamano dhidi ya Israel.
Mmoja ya raia wa Palestina katika moja ya maandamano dhidi ya Israel. MOHAMMED ABED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hakuna uchaguzi wowote ambao umefanyika huko Gaza, Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki kwa miaka kumi na tano.

Makundi mawili makubwa, Fatah ya rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na Hamas, kundi la Waislam wenye silaha ambao wanapinga mazungumzo yoyote na Israeli, walikubaliana Jumatatu kukutana jijini Cairo, nchini Misri, kujiandaa kwa uchaguzi wa wabunge wa Mei 22 na uchaguzi wa urais Julai 31.

Makundi hayo mawili makubwa na makundi mengine madogo 12 ya Wapalestina yameahidi katika taarifa yao "kufuata kalenda ya uchaguzi" na "kuheshimu na kukubali" matokeo ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.