Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-AFGHANISTAN-MAUAJi-USALAMA

Australia yahusishwa kwa mauaji ya raia 36 kutoka Afghanistan

Vikosi maalum vya kijeshi kutoka Australia, viliwauwa raia na wafungwa 39 wa Afganistan kinyume cha sheria, ikiwa ni kama utamaduni wao wa kukaribishwa vitani, kwa mujibu wa uchunguzi wa kijeshi.

Australia ilituma wanajeshi wake wapatao Elfu 26 nchini Afganistan kwenda kupambana na sambamba na wanajeshi wa Marekani dhidi ya makundi ya Taliban na Al Qaeda baada ya shambulizi la kigaidi mwaka 2001 nchini Marekani.
Australia ilituma wanajeshi wake wapatao Elfu 26 nchini Afganistan kwenda kupambana na sambamba na wanajeshi wa Marekani dhidi ya makundi ya Taliban na Al Qaeda baada ya shambulizi la kigaidi mwaka 2001 nchini Marekani. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa mauaji hayo wenye kurasa 465, umeonesha mauaji hayo yalitokea kati ya mwaka 2005-2016 na sasa ripoti hiyo imekabidhiwa kwa mwendesha mashtaka maalum wa uhalifu wa kivita nchini Australia.

Imebainika kuwa wanajeshi wa Australia wamekuwa wakishiriki katika mauaji haya ya kiholela, jambo ambalo mkuu wa majeshi nchini humo amekiri na kusema ni vitendo ambavyo havikubaliki.

Mkuu huyo wa majeshi, Angus Campbell ameongeza kuwa, hakuna mauaji yaliyotokea  kwenye mazingira ya kivita, na wanajeshi waliohusika na kuulizwa walikuwa wanafahamu vema kuhusu kanuni za vita.

Ripoti hiyo inapendekeza watu 19 kushatakiwa, familia za waathiriwa walipwe fidia lakini pia kuwe na mageuzi katika jeshi la nchi hiyo.

Australia ilituma wanajeshi wake wapatao Elfu 26 nchini Afganistan kwenda kupambana na sambamba na wanajeshi wa Marekani dhidi ya makundi ya Taliban na Al Qaeda baada ya shambulizi la kigaidi mwaka 2001 nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.