Ajali ya ndege ya watu zaidi ya 11 Pakistani
Ndege ya Shirika la kimataifa la ndege la Pakistani, Pakistan International, imeanguka katika makazi ya watu ya Model Colony huko Karachi, nchini Pakistani, vyanzo vya usalama vimebaini.
Imechapishwa:
Mamlaka ya usimamizi wa safari za ndege nchini Pakistan, imesema kuwa, ndege hiyo iliyoanguka wakati ikitua na kulipuka huku makaazi ya watu yakiteketea kwa moto.
Msemaji wa Mamlaka hayo Abdullah Hafeez amesema kuwa abiria 91 na wafanyikazi saba ndio waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyopoteza mwelekeo.
Hadi sasa, mamlaka ya safari za ndege nchini humo inasema, uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo lakini maneno ya mwisho ya rubani huyo, alisikika akisema kuna hitilafu ya kimitambo
Kabla ya kuanguka, ndege hiyo ilikuwa imeondoka mjini Lahore, ikielekea katika mji wa Karachi, mji mkubwa nchini humo.