Pata taarifa kuu
PAKISTANI-AJALI-USALAMA

Watu zaidi ya 17 wauawa baada ya ndege ya jeshi kuanguka Pakistani

Watu zaidi ya 17 wamefariki dunia mapema Jumanne asubuhi wakati ndege ndogo ya jeshi la Pakistani imeanguka katika eneo la makazi la Rawalpindi, mji ulio karibu na mji mkuu wa Islamabad, afisa wa idara ya huduma za dharura ameliambia shirika la Habari la AFP.

Wanajeshi wa Pakistani katika makao yao makuu ya Rawalpindi Oktoba 10, 2009.
Wanajeshi wa Pakistani katika makao yao makuu ya Rawalpindi Oktoba 10, 2009. REUTERS/Faisal Mahmood
Matangazo ya kibiashara

"Tumepokea miili 17 ikiwa ni pamoja na raia 12 na wafanyakazi 5 wa ndege hiyo. Watu 12 wamejeruhiwa," amesema msemaji wa idara ya huduma za dharura Farooq Butt. Ripoti ya awali ilibaini kwamba watu 15 ndio waliuawa katika ajali hiyo.

Ajali hiyo ilitokea mapema alfajiri katika kitongoji cha mji wa Rawalpindi, ambao pia ni makao makuu ya jeshi la Pakistani. Eneo hilo lilizingirwa haraka na vikosi vya usalama, huku magari ya wagonjwa mahututi yakitumwa eneo la tukio.

Jeshi katika taarifa yake, limesema kuwa ndege iliyoanguka ilikuwa ndege ya mafunzo ambayo ilikuwa katika "mafunzo ya kawaida" wakati wa ajali hiyo, na kuthibitisha kuwa wafanyakazi watano wa ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na marubani wawili walikuwa katika ndege hiyo. Waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.