Pata taarifa kuu
PALESTINA-EU-USHIRIKIANO

Kiongozi wa Palestina azuru Ubelgiji

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas amezuru jijini Brussels nchini Ubeljini kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya, na kuwaambia watambue Palestina kama taifa.

Mahmoud Abbas na Federica Mogherini katika mkutano wao na waandishi wa habari  Brussels Jumatatu 22 Januari 2018.
Mahmoud Abbas na Federica Mogherini katika mkutano wao na waandishi wa habari Brussels Jumatatu 22 Januari 2018. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Rais Abbas ambaye amekutana na Mkuu wa sera za Mambo ya nje ya Umoja huo Federica Mogherini kuwa Wapalestina bado wanataka amani ya muda mrefu katika Mashariki ya Kati, na kuitaka Umoja huo kuchukua usakani wa kusimamia hilo.

Mogherini amemwambia Abbas kuwa, Umoja wa Ulaya bado una nia ya dhabti kuunga mkono Mashariki mwa Jerusalem kuwa mji wake mkuu katika siku zijazo.

Kauli hii inakuja siku moja baada ya Marekani kusema kuwa, itahamisha ubalozi wake nchini Israel kutoka mjini Tel Aviv kwenda Jerusalem mwisho wa mwaka 2019.

Tangazo hili lilitolewa na Makamu wa rais Mike Pennce, baada ya ziara yake nchini Israel na kulihotubia bunge.

Wakati wa hotuba hiyo, wabunge wenye asili ya kiarabu walianza kumzomea na kumlazimu Spika kuwaondoa bungeni.

Waziri Mkuu Benjamin Netayanhu amesema, Marekani imeonesha kuwa ni rafiki wa dhati wa Israel kutokana na uamuzi wake wa kuhamisha ubalozi wake na kutambua Jerusalem kuwa makao makuu ya nchi hiyo, licha ya pingamizi kubwa Kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.