Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN-USALAMA

Mlipuko waua mtu mmoja karibu na Ubalozi wa Marekani Afghanistan

Mlipuko ulisikika Jumatano hii asubuhi karibu kituo cha umeme cha ubalozi wa Marekani mjini Kabul, mamlaka nchini Afghanistan imesema.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikikagua eneo kulikotokea mlipuko wa vurugu Kabul. Mlipuko amabao umeua lmtu mmoja na kuwajeruhi wengine wanne Jumanne Agosti 29 karibu na ubalozi wa Marekani.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikikagua eneo kulikotokea mlipuko wa vurugu Kabul. Mlipuko amabao umeua lmtu mmoja na kuwajeruhi wengine wanne Jumanne Agosti 29 karibu na ubalozi wa Marekani. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea mbele ya benki, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Najib Kidenmaki.

Wizara ya afya imetangaza kwamba mlipuko huo umesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wanane wamejeruhiwa.

Mabenki ya mji mkuu wa Afghanistan yanatembelewa na watu wengi siku chache kabla ya Siku Kuuu ya Kiislamu ya Eid Adha'a.

Eneo hili mjini Kabul limekua mara kwa mara likilengwa na mashambulizi. Mnamo mwezi Juni, mlipuko wa bomu lililotegwa katika lori ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 150 katika eneo hili.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza wiki iliyopita kuendelea kwa ushirikiano wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.