Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MASHAMBULIZI

Syria: watu 148 wauawa katika mashambulizi ya IS

Serikali ya Syria imekumbwa na mfululizo wa mashambulizi na kuua watu 148 katika ngome zake katika mkoa wa pwani. Kundi la Islamic State limedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Askari na raia kutoka jeshi la Syria wakikagua uharibifu baada ya milipuko iliyoukumba mji wa Syria wa Tartous, Mei 23 2016.
Askari na raia kutoka jeshi la Syria wakikagua uharibifu baada ya milipuko iliyoukumba mji wa Syria wa Tartous, Mei 23 2016. SANA/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yalioyakumba maeneo yaTartous na Jableh ni mapya katika miji hiyo inayokaliwa kwa kiasi kikubwa na watu kutoka jamii ya watu wachache, ambayo ni jamii ya rais wa Syria Bashar al-Assad. Miji hii imekua imetengwa na vita vinavyoendelea nchini Syria kwa miaka mitano sasa.

Moja ya mashambulizi imetekelezwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alilipua mkanda wake uliokua umejaa vilipuzi katika hospitali ambako alikuwa akisaidia kubeba majeruhi wa mlipuko wa bomu lilotegwa ndani ya gari kabla ya tukio hilo kutokea, kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na shirika la haki za binadamu la Syria (OSDH).

Mfululizo huu wa kipekee wa mashambulizi umeendeshwa wakati ambapo kundi la Islamic State limeendelea kuonekana dhaifu nchini Syria na Iraq, ambapo vikosi vya serikali vimeanzisha Jumatatu hii vita kwa lengo la kuwatimua wanajihadi katika mji wa Fallujah.

Wakati huo huo kundi la Islamic State pia limedai kutekeleza mashambulizi mawili nchini Yemen yaliyogharimu maisha ya watu wasiopungua 41, mashambulizi ambayo yamewalenga vijana walioajiriwa katika jeshi mjini Aden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.