Pata taarifa kuu
PAKISTAN-MAUAJI-MAANDAMANO

Pakistan: watu zaidi ya 65 wauawa katika shambulizi Lahore

Nchini Pakistan, kumetokea shambulio la kujitoa mhanga katika hifadhi ya mji wa Lahore. Polisi imebaini kwamba watu wasiopungua 65 wameuawa na wengine zaidi ya mia moja wamejeruhiwa. Hili ni shambulio baya la kujitoa mhanga kuwahi kutokea kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa nchini humo.

Shughuli za uokozi zaendelea katika eneo la shambulio katika hifadhi ya Lahore, Machi 27, 2016.
Shughuli za uokozi zaendelea katika eneo la shambulio katika hifadhi ya Lahore, Machi 27, 2016. ARIF ALI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wetu, katika mji wa Islamabad, Michel Picard, mtu aliyekua amevaa mkanda wa kulipuka alijilipua katika mlango wa hifadhi katika eneo la makazi ya mji wa Lahore. Mji mkuu wa Punjab bado ni moja ya miji maarufu ilio salama nchini humo.

Mshambuliaji amejilipua katikati ya umati wa watu waliokuwa wakiondoka katika hifadhi hiyomapema Jumapili hii jioni, siku moja kabla ya kuhitimishwa likizo za shule. Mashahidi wanasema matukio ya kutisha ya vipande vya miili ya binadamu vimetawanyika pembezoni mwa hifadhi ya Gulshan-e-Iqbal. Kwa mujibu wa shahidi mwingine, kulikuwa na ukaguzi mdogo wa usalama katika hifadhi hiyo na maeneo jirani.

Wahamga ni hasa wanawake na watoto ambao wana kawaida nchini Pakistan kutembelea Jumapili mchana katika bustani za manispaa. Hospitali za mji huo ziko katika hali ya dharura, magari kadhaa ya wagonjwa yako eneo hilo na idadi kubwa ya askari polisi imetumwa katika eneo hilo la tukio.

Kundi moja lenye mafungamano na kundi la Taliban nchini Pakistan limekiri kuhusika na shambulizi hilo. Kundi hilo limebaini kwamba shambulizi hilo limekua limewalenga Wakristo waliokua wakisheherekea siku kuu ya Pasaka katika hifadhi ya manispa ya jiji la Lahore.

Siku hii ya Jumapili pia kumeshuhudiwa maandamano makubwa katika mji wa Islamabad, maandamano yaliwajumuisha wafuasi wa mwanaharakati wa Kiislam alienyongwa mwishoni mwa mwezi Februari kwa kosa la kumuua mkuu wa mkoa wa Punjab mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.