Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-HIJJA-USALAMA

Riyadh yakataa kutwishwa mzigo wa makosa katika ibada ya Hija

Mfalme Salaman wa Saudi Arabia amefutilia mbali Jumatatu wiki hii tuhuma dhidi ya nchi yake katika maandalizi ya ibada ya Hija ya kila mwaka kwa Waislamu katika mji mtakatifu wa Makka, baada ya mkanyagano uliyosababisha vifo vya watu wengi Septemba 24 mwaka huu.

Miili ya watu waliofariki baada ya kukanyagana katika mji wa Makka, Septemba 24, 2015, Saudi Arabia.
Miili ya watu waliofariki baada ya kukanyagana katika mji wa Makka, Septemba 24, 2015, Saudi Arabia. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

" Taarifa isiyo sahihi inayolenga kuchochea kisiasa ajali hii na kugawanya ulimwengu wa Kiislamu, yote hayo hayana athari kwenye jukumu, wajibu na majukumu makubwa kwa ufalme wa Saudi Arabia wa kutumikia mahujaji ", amesema mfalme, ambaye ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Riyadh, kwa mujibu wa shirika la habari la SPA.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Saudi Arabia, mkanyagano mkubwa wa Septemba 24 katika mji mtakatifu wa Mina, karibu na mji mtakatifu wa Makka, uliwaua watu 769.

Lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na nchi 30, idadi ya watu waliofariki katika ajali hiyo, imeongezeka Jumatatu wiki hii na kufikia watu 1608, ikiwa ni ajali mbaya kuwahi kutokea katika historia ya ibada ya Hija.

Mara tu baada ya ajali hiyo, nchi nyingi zilitoa hisia zao, hasa Iran, yenye watu wengi kutoka Dhebu la Shia, ikiwa pia mpinzani wa ufalme wa Saudi, kwa kuwashtumu maafisa wa Saudi Arabia kuwa walifanya uzembe na urasibu mbaya katika kuandaa mkusanyiko mkubwa wa kila mwaka wa Waislamu.

Nchini Uturuki, kiongozi mmoja wa wa chama tawala cha Kiislamu cha kihafidhina alipendekeza kuwa nchi yake iandae ibada ya Hija kwa sababu " maeneo takatifu ya Uislamu ni mali ya Waislamu wote ", maneno ambayo Rais Recep Tayyip Erdogan aliyapinga mara moja.

Mfalme Salman, ambaye amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya nchi yake kukosolewa, amesema mbele ya Baraza la mawaziri kwamba " ufalme kamwe hautoruhusu mtu yeyote kukashifu na kuweka lawama nchi yake katika maandalizi ya ibada ya Haji."

Mfame nchi Saudi Arabia ni "mlinzi wa Miskiti miwili Mitakatifu", maeneo matakatifu ya Makka na Madina, magharibi mwa Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.