Pata taarifa kuu
PALESTINA-IS-ICC-UHALIFU-SHERIA-HAKI

Uhalifu wa kivita: Wapalestina wawasilisha faili ICC

Wapalestina wamewasilisha Alhamisi wiki hii faili yao ya kwanza mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ambapo wanaituhumu Israeli kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Wana matumaini kuwa watamshinikiza Mwendesha mashitaka wa ICC kuanzisha uchunguzi.

Wapalestina wanaituhumu Israeli vifo vya zaidi ya watoto 500 wakati wa vita Gaza katika majira ya joto 2014.
Wapalestina wanaituhumu Israeli vifo vya zaidi ya watoto 500 wakati wa vita Gaza katika majira ya joto 2014. FP PHOTO / MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Ramani, takwimu, hata picha za satelaitini vielelezo ambavyo Wapalestina wametoa kama nyaraka sahihi kwa ICC zinazolaani kile wanachokiona kuwa ni uhalifu wa kivita uliyotekelezwa na Israel.

Mapema Leo Alhamisi Mustafa Barghouti, mjumbe wa kamati ya Palestina kwa ICC amesema: " Faili ambayo tutawasilisha itaonyesha kuwa ukiukaji uliyotekelezwa na Israel ni wenye kuendelea, na ukiukwaji huo ni matokeo ya sera iliyopangwa kwa upana, kwa kukusudia kuwaangamiza Wapalestina .

" Lengo letu ni kuthibitisha kuwa uhalifu mkubwa ulitekelezwa, na unatisha ili ICC ianzishe uchunguzi. Tutaonyesha ushahidi wa kile kilichotokea katika suala nzima la uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Tutaonyesha jinsi gani viongozi waandamizi wa jeshi la Israel, viongozi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na siasa na uchumi nchini Israel,walivyojihusisha na uhalifu dhidi ya raia wa kawaida", ameongeza Mustafa Barghouti.

Ukoloni na watoto waliouawa Gaza

Moja ya mada zilizowasilishwa kwenye faili hiyo ni ukoloni wa Israel. " Ukoloni wenyewe ni uhalifu na uvunjaji wa sheria za kimataifa, kwa sababu ukoloni ni kitendo kichafu ambacho kinahusu kuwapokonya Wapalestina ardhi zao, na kulazimisha watu kuyahama makaazi yao kwa faida ya walowezi, sera ambayo iliyoanzishwa na serikali ya Israel bila ya sheria za kimataifa ", amesema Mustafa Barghouti.

Uhalifu mwingine uliyotekelezwa na Israel, kwa mujibu wa Wapalestina: vifo vya watoto zaidi ya 500 wakati wa vita katika mji wa Gaza mwaka mmoja uliopita. " Umoja wa Mataifa ulitoa taarifa ya matukio kama vile yale ya mtoto mwenye umri wa miaka 6 aliyejeruhiwa tumboni huku akishikilia matumbo yake. Mtoto huyo aliomba msaada bila mafanikio. Alifariki kutokana na tabia mbaya ya Israel. Israel haiwezi kuepuka na kuhusika kwake katika uhalifu huu wa kivita ", ameendelea kusema Mustafa Barghouti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.