Pata taarifa kuu
JORDAN-UINGEREZA-Sheria

Mhubiri wa Kiislam Abu Qatada, aachiwa huru Jordan (Sheria)

Mhubiri wa dini ya kiislam Abou Qatada ameachiliwa huru baada ya kukutwa hana hatia kwa tuhuma za ugaidi zilizokua zinamkabili. Mhubiri huyo alihukumiwa na kufungwa nchini Uingereza kwa kosa la ugaidi na baadae kusafirishwa hadi nchini Jordan mwezi Julai mwaka 2013.

Imam mwenye itikadi kali za dini, Abou Qatada,  ambae anajulikana kama mshirika wa karibu wa ben Laden  Barani Ulaya.
Imam mwenye itikadi kali za dini, Abou Qatada, ambae anajulikana kama mshirika wa karibu wa ben Laden Barani Ulaya. Reuters / Handout/Files
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Jordan, akijulikana kwa jina lake halisi la Omar Mahoud Othmane ameondolewa katika jela la Mouaqqar jumatano alaasiri wiki hii (kwenye umbali wa kilomita 45 na mji mkuu wa Jordan Amman), ambako ndugu, jamaa na marafiki zake wamekua wakimsubiri, kabla ya kujielekeza nyumbani kwake mjini Amman.

Abou Qatada alihukumiwa nchini Jordan mbele ya Korti ya salama wa taifa tangu aliposafirishwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka 2013 kufuatia changa moto za kidiplomasia na sheria kwa takribani miaka 10.

Korti hiyo imefuta tuhuma dhidi ya Abou Qatada na kuamuru aondolewe jela baada ya kukutwa kuwa hana hatia. Raia huyo wa Jordan alituhumiwa kuhusika na shambulio la kigaidi dhidi ya watalii mwaka 2000, lakini Korti hiyo imeamuru mhubiri huyo achiwe huru mara moja, chanzo cha usalama ambacho kiliomba jina lake lihifadhiwe kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Korti hiyo imebaini kwamba haikupata vithibitisho vya kutosha kuhusu tuhuma dhidi ya Abou Qatada, kwa hiyo tuhuma dhidi yake imefutwa na ataachiwa huru, chanzo hicho kimeeleza.

Baada ya tangazo la uamzi wa korti, mhubiri huyo ametokwa na machozi, huku ndugu, jamaa na marafiki zake waliohudhuria kesi hiyo wakimpongeza Mwenye- Enzi-Mungu, wakisema Mwenye-Enzi-Mungu ni mkubwa.

Abou Qatada akifumbatiwa na baba yake son père alitoka jelaSeptemba 24 mwaka 2014 Jordan.
Abou Qatada akifumbatiwa na baba yake son père alitoka jelaSeptemba 24 mwaka 2014 Jordan. REUTERS/Muhammad Hamed

Mwanasheria wake, Hussein Mbidhine amepongeza uamzi wa Korti na kusema vyombo vya sheria nchini Jordan vimeonesha kuwa ni jasiri.

Mwezi Juni Abou Qatada alifutia tuhuma ya kushiriki katika kuandaa kitendo cha ugaidi dhidi ya shule moja inayomilikiwa na Marekani mjini Amman, baada ya kukosa ushahidi tosha, lakini aliendelea kusalia gerezani kwa tuhuma zingine za ugaidi.

Hata hivo, serikali ya Uingereza imekataa katu katu kurejea kwa Abou Qatada nchini Uingereza. “ Hatutaki kabisa mtu huyo kurejea nchini Uingereza” aliwahi kusema naibu Waziri Mkuu, Nick Cleg

Kauli hiyo imeungwa mkono jumatano wiki hii na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, ambapo amesema kuwa Abou Qatada anakabiliwa na vikwazo vya kutosafiri viliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa, akibaini kwamba hawezi kuthubutu kurejea Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.