Pata taarifa kuu
IRAQ

Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Maliki akataa wito ya kuunda serikali ya pamoja

Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Maliki amekataa wito wa kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kama mbinu ya kufanikiwa kusitisha mapigano ya Wasunni nchini humo.

Waziri Mkuu wa Iraq  Nouri al-Maliki.
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki. AFP PHOTO / Ahmed Saad / POOL
Matangazo ya kibiashara

Maliki ambaye amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa ikiongozwa na Marekani ameonya kuwa uundwaji wa serikali kama hiyo itakuwa kinyume cha Katiba na itasababisha mgogoro wa kidemokrasia nchini humo.

Kauli ya Maliki inakuja wakati huu kundi la kwanza la wanajeshi wa Marekani limewasili nchini Iraq kuwashauri wanajeshi wa nchi hiyo namna ya kupambana na kuwashinda wapiganaji wa Kusunni wa ISIL wanaopambana na serikali.

Wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq
Wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq REUTERS/ Ako Rasheed

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwasili kwa wanajeshi hao juma moja baada ya rais Barrack Obama kuahidi kuwa itatuma wanajeshi 300 kuwashauri wanajeshi wa Iraq.

Waziri wa Mambo wa Marekani John Kerry amekuwa ziarani nchini Iraq kuzungumza na viongozi wa juu wa nchi hiyo akiwemo Waziri Mkuu Nuri al-Maliki kuona namna ya kusitisha mapigano hayo kwa kuwashiwishi viongozi wa nchi hiyo kuunda serikali ya pamoja.

Wanajeshi wa Marekani 40 tayari wapo mjini Baghdad, kuchunguza hali ya mambo katika uwanja wa mapambano.

Wanajeshi wa Iraq  wakipambana na wapiganaji wa ISIL
Wanajeshi wa Iraq wakipambana na wapiganaji wa ISIL Reuters/路透社

Pentagon inasema wanajeshi wengine 90 watakuwa jijini Baghdad kuweka Operesheni ya pamoja na wanajeshi wa Iraq katika harakati za kupambana na wapiganaji hao ambao wanadhibiti miji ya Kaskazini na Magharibi mwa nchi hiyo.

Wanajeshi zaidi wa Marekani wanatarajiwa kujiunga na wenzao katika siku kadhaa zijazo kuona namna ya kulisaidia jeshi la Iraq kuwashinda wapiganaji hao.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa, vita vya Iraq vimesababisha vifo vya watu 1,075 mwezi wa Juni pekee, wengi wao wakiwa raia wa kawaida.

Wapiganaji wa Kisuni
Wapiganaji wa Kisuni REUTERS/Alaa Al-Marjani

Siku ya Jumatano, kundi la kigaidi la Al-Qaeda lilitangaza kuwa limejiunga na kundi hilo la ISIL na linadhibiti mji wa Levant karibu na mpaka wa Syria.

Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema muunngano huu utawapa nguvu kundi la ISIL a kudhibiti mji wa Albu Kamal nchini Syria na Al Qaim nchini Iraq na kuendelea kusonga mbele.

Viongozi wa muungano wa majeshi ya nchi za Magharibi NATO wanakutana jijini Brussels nchini Ubelgiji, katika kikao hicho ambacho pia kinahudhuriwa  na Kerry kuthathmini hali ya makabiliano nchini Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki  ameiomba Marekani kutuma ndege zake zisozokuwa na rubani kupambana na wapiganaji hao.

Wapiganaji hao wanataka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Maliki na wanasema wanapigania taifa la Kislamu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.