Pata taarifa kuu
IRAN

Iran yaadhimisha miaka 34 ya mapunduzi ya kiislamu yaliyoangusha utawala uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani

Mamilioni ya waumini wa dini ya kiislamu nchini Iran wamejitokeza kushiriki maandamano ya kuadhimisha miaka thelathini na nne ya mapinduzi ya kiislamu nchini humo yaliyofanikisha kuangushwa kwa serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani ya Rais Shah Mohamed Reza Pahlavi na kuifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri mnamo februari 11 mwaka 1979.

© Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yameshika kasi zaidi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bahrain na katika miji mingine ya Mashhad, Isfahan, Shiraz na Kerman.

Rais wa nchi hiyo Mahmud Ahmedinejad amehutubia mamilioni ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa serikali wa Azad huku akiionyooshea kidole Marekani na kusema inapaswa kubadili kwanza msimamo wake kama inataka kufanya mazungumzo ya mpango wa nyuklia na Taifa hilo.

Bendera za Taifa hilo zimepaishwa katika miji mbalimbali huku jina la kiongozi wa mapinduzi hayo Ayatollah Ruhollah Khomein likitawala katika mabango mbalimbali yaliyobebwa na waandamanaji kama ishara ya pongezi kwa kufanikisha mapinduzi hayo.

Iran kwa sasa inakabiliwa na vikwazo kutokana na mpango wake tata wa nyuklia ambao unapata upinzani mkali wakati idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaunga mkono mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.