Pata taarifa kuu
DRC-UN

UN yaitaka Serikali ya DRC kuandaa mpango wa kuwanyang'anya silaha makundi mengine ya waasi

Umoja wa Mataifa UN umeitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha makundi mengine ya waasi wanasalimisha silaha pamoja na kuwashirikisha kwenye jeshi la nchi hiyo. 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon (Kushoto) akiteta na rais Joseph Kabila hivi karibuni alipofanya ziara nchini DRC
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon (Kushoto) akiteta na rais Joseph Kabila hivi karibuni alipofanya ziara nchini DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tamko la Umoja wa Mataifa linatolewa wakati huu ambapo kikosi maalumu cha umoja huo kilichoko mashariki mwa nchi ya DRC kwa kushirikiana na wanajeshi wa Serikali FARDC walifanikiwa kuwafurusha wapiganaji waasi wa kundi la M23.

Operesheni hiyo ilifanikisha kumaliza uasi wa kundi la M23 uliokuwa umedumu kwa zaidi ya miezi kumi na minane ambapo mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makazi yao.

Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Kongo, Abdallah Wafi amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango huo ni muhimu kwa Serikali ya Kinshasa kama njia mojawapo ya kufikia suluhu ya amani mashariki mwa nchi hiyo.

Baadhi ya wapiganaji wa kundi la M23 walijisalimisha kwa vikosi vya Umoja huo na wengine kukimbilia Rwanda kuomba hifadhi jambo ambalo pia huenda likasababisha wapiganaji waliosalia na ambao hawajasalimisha silaha kujikusanya tena.

Katika hatua nyingine jeshi la Serikali ya DR Congo limesema hivi sasa linajipanga kuanza mashambulizi mapya dhidi ya wapiganaji wa Kinyarwanda wa kundi la FDLR ambao wakati fulani walipigana na Serikali mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.