Pata taarifa kuu
UN-CLIMATE CHANGE

Viongozi wa mataifa wakutana mjini Warsaw, Poland kujadili mabadiliko ya tabia nchi

Nchi wanachama kwenye Umoja wa Mataifa, UN hii leo wameanza mkutano wao mjini Warsaw nchini Poland, kujadili mabadiliko ya tabia nchi wakati huu dunia ikikabiliana na ongezeko la hali joto na ongezeko la hewa ya ukaa. 

Moja ya maeneo barani Afrika yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
Moja ya maeneo barani Afrika yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Nchi wanachama zinakutana wakati huu ambapo nchi ya Ufilipino imekumbwa na madhara makubwa yaliyotokana na kimbunga cha Typhoon Haiyan ambacho kwa sehemu kubwa kimeelezwa kusababishwa na uharibifu wa mazingira.

Mkutano huu wa siku kumi na mbili kwenye Umoja wa Mataifa unawakutanisha wadau wa mazingira duniani pamoja na mawaziri wa mazingira toka nchi mbalimbali duniani kujadili namna ya kukabiliana na hali joto duniani.

Mkuu wa masuala ya hali ya hewa kwenye Umoja wa Mataifa, Christiana Figueres amewaonya viongozi wa dunia kuhusu hali inayoshuhudiwa hivi sasa na kwamba iwapo hawatachukua hatua za kudhibiti uharibufu wa mazingira unaofanywa na binadamu.

Mkuu huyo ameongeza kuwa athari za hali joto duniani zinazoshuhudiwa kwasasa kwa sehemu kubwa zinachangiwa na shughuli za kibinadamu ambapo iwapo hatua hazitachukuliwa mapema hali ambayo huenda ikawa mbaya zaidi.

Ameongeza kuwa kinachoshuhudiwa nchini Ufilipino na maeneo mengine ya dunia na hata sehmu zenye ukame ni madhara yanayotokana na uharibufu wa mazingira na kukosekana kwa sheria madhubuti kukabiliana na hali hii.

Mkutano huu unafanyika wakati huu ambapo mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani yakivutana kuhusu namna ya kukabiliana na ongezeko la hewa ukaa kwenye uso wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.