Pata taarifa kuu
TANZANIA-TANZIA-SIASA

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Augustine Mahiga afariki dunia

Waziri wa Katiba na Sheria , Balozi Dkt Augustine Mahiga amefariki dunia alfajiri ya leo baada ya kuugua ghafla akiwa mjini Dodoma. viongozi mbalimbali katika serikali ya Tanzania wanaendelea ktuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu.

Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga, kushoto, (wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Richard Sezibera wakati wa majadiliano kuhusu mazungumzo ya Burundi huko Arusha
Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga, kushoto, (wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Richard Sezibera wakati wa majadiliano kuhusu mazungumzo ya Burundi huko Arusha Filbert Rweyemamu / AFP
Matangazo ya kibiashara

Balozi Mahinga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Na amefikishwa hospitali akiwa ameshafariki dunia.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Wafanyakazi wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Tanzania imempoteza mtu muhimu kwa taifa hilo ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kwa ujenzi wa nchi hiyo.

Rais Magufuli amemueleze Marehemu Balozi Mahiga kuwa alikuwa mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri, aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za kimataifa kwa miaka mingi.

“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalumbali za kitaifa na kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa myenyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma”, amesema rais wa Tanzania.

Balozi Mahiga ambaye alizaliwa Agosti 28 mwaka 1945, alikuwa mwanadiplomasia wa muda mrefu wa Tanzania na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kutoka mwa 2015 hadi 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.