Pata taarifa kuu
KENYA-BUNGE-SIASA-JINSIA-WANAWAKE

Mswada wa kuongeza idadi ya wanawake bungeni nchini Kenya wajadiliwa

Wabunge nchini Kenya wanajadili mswada unaolenga kuongeza idadi ya wanawake na kuhakikisha kuwa kuna usawa wa jinsia katika bunge la taifa na lile la Senate, kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 2010.

Wabunge nchini Kenya, katika kikao kilichopita
Wabunge nchini Kenya, katika kikao kilichopita www.parliament.go.ke
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Juu nchini humo iliagiza bunge kutunga sheria ili kutekeleza agizo hilo la Katiba, kuhakikisha kuwa jinsia moja haizidi thuluthi mbili katika nafasi zote za uteuzi.

Mswada huu mpya unaopendekezwa na kiongozi wa serikali bungeni Aden Duale, na unakuja baada ya wabunge wanawake mara tatu, kutofanikiwa kuwashawishi wabunge wa kiume kuwaunga mkono.

Viongozi wa juu wa serikali, wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, wametoa wito kwa wabunge kuupitisha mswada huo ili kutoa nafasi kwa wanawake zaidi kuingia bungeni.

Kati ya wabunge 290 nchini Kenya, kwa sasa wabunge wanawake waliochaguliwa ni 22 na 50 wateule na kufanya idadi yao kufika 75.

Iwapo mswada huu utapitisha idadi hiyo ya wanawake, inatarajiwa kuongezeka na kufikia zaidi ya 100.

Kenya ni ya mwisho katika ukanda wa Afrika Mashariki, kwa wanawake walio bungeni.

Rwanda ni ya kwanza kwa asilimia 61, Tanzania ni ya pili kwa asilimia 36 sawa na Burundi, huku Uganda ikiwa na asilimia 34 na Kenya ikiwa na asilimia 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.