Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI

Miili 126 yaopolewa kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere, nchini Tanzania

Watu 126 wamethibitika kupoteza maisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuyko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake ndani ya Ziwa Victoria, nchini Tanzania.

Juhudi za kunasua miili zinaendelea Ziwani Victoria, nchini Tanzania kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere
Juhudi za kunasua miili zinaendelea Ziwani Victoria, nchini Tanzania kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere http://www.mwananchi.co.tz/
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za uongezeko la watu waliopoteza maisha limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Mhandishi Isack Kamwele, alipozungumza na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Taarifa hizi zinafuatia zoezi la kunasua miili ambalo lilianza leo asubuhi baada ya kusitishwa jana, kufuatia kuingiza kwa kiza.

Ferry hiyo MV Nyeyere iliyokuwa imewababe mamia ya abiria, ilizama ikitokea katika kisiwa cha Bugorora kwenda katika kisiwa kingine cha Ukara katika Wilaya ya Ukerewe.

Ripoti zaidi zinasema zoezi hilo litaendelea hadi jioni ya leo ambapo serikali ya Tanzania itatoa taarifa rasmi kuhusu juhuzi za kunasua miili ya watu waliopoteza maisha.

Katika hatua nyingine, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na rais wa Rwanda, Paul Kagame wametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Tanzania kufuatia msiba huo mzito.

Ripoti zaidi zinasema familia za watu waliopoteza maisha wamekuwa wakifika hatika hospitali ya Biswa, kutambua miili ya jamaa zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.