Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA-HAKI

Bobi Wine kurejea Kampala

Mbunge wa upinzani aliyechaguliwa katika eneo la Kyandodo Mashariki mwa Uganda, na mwanamuziki maarufu Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine ameyaambia magazeti ya Mail na Guardian kuwa yuko tayari kurudi nchini Uganda siku ya Jumatatu.

Mwanamuziki maarufu na Mbunge Robert Kyagulanyi, anayefahamoka kwa jina la Bobi Wine, katika mkutano na waandishi wa habari na wakili wake huko Washington, DC, Septemba 6, 2018.
Mwanamuziki maarufu na Mbunge Robert Kyagulanyi, anayefahamoka kwa jina la Bobi Wine, katika mkutano na waandishi wa habari na wakili wake huko Washington, DC, Septemba 6, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Uganda kwa sasa yupo Marekani anapopatiwa matibabu baada ya kupigwa na maafisa wa usalama wa Uganda amesema licha ya hofu ya kukamatwa na kufanyiwa madhila mengine ameamua kurudi nyumbani kutetea wanyonge.

“Punde tu madaktari wangu wataniruhusu nitatarudi Uganda kuendelea na harakati za kisiasa” amesema Bw Kyagulanyi.

Robert Kyagulanyi, ambaye amekua mwiba kwa utawala wa Yoweri Museveni amesema hali yake inaendelea vizuri na anatamani kukutana na wafuasi wake.

Robert Kyagulanyi alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka uliyopita wilayani Kyadondo mashariki, mwa Uganda.

Bobi Wine na wenziwe 32 walikamatwa baada ya kudaiwa kushambulia msafara wa Rais wa Yoweri Museveni mjini Arua mwezi uliopita na kuwekwa katika kizuizi cha jeshi.

Mwanzo alipandishwa katika mahakama ya kijeshi kabla ya kuhamishiwa kwenye mahakama ya kiraia na kushtakiwa kwa kosa la uhaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.