Pata taarifa kuu
KENYA-EU

Bunge la Ulaya kujadili hali ya kisiasa nchini Kenya

Bunge la Ulaya litajadili hali ya kisiasa nchini Kenya siku ya Jumanne, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 na hasa baada ya waangalizi kutoka Umoja huo kutoa ripoti kuhusu walichokithathmini katika Uchaguzi huo.

Bunge la Umoja wa Ulaya
Bunge la Umoja wa Ulaya euobs-media
Matangazo ya kibiashara

Mjadala huu umethibitishwa na aliyekuwa kiongozi wa waangalizi hao Marietje Schaake, ambaye wiki iliyopita alitoa ripoti ya kina kuhusu walichokishuhudia nchini Kenya.

Ripoti ya waangalizi hao ilieleza kuwa wanasiasa kutoka pande zote, walitumia fedha kuwahonga wananchi wa taifa kuhuduria mikutano ya kisiasa lakini pia fedha za umma zilitumiwa katika kampeni hiyo.

Wanasiasa nchini Kenya pia walishtumiwa kwa kutoa matamshi ya kuitishia Tume ya Uchaguzi na kusababisha wapiga kura kutofanya uamuzi wao kwa uhuru.

Ripoti hiyo ilitolewa jijini Brussels, baada ya kusema kuwa walizuiwa na serikali ya Kenya kuja jijini Nairobi baada ya kukataa ripoti hiyo.

Wakati mjadala huu ukifanyika, viongozi wa muungano wa upinzani NASA wameendelea kukutana kujadili kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga tarehe 30 mwezi huu kama rais wa watu, lakini pia uwezekano wa kuwa na mazungumzo.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye hajamaliza kulitangaza Baraza lake la Mawaziri, tayari amesema yuko tayari kwa mazungumzo lakini yawe yanalenga maendeleo ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.