Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Sudan Kusini: Maelfu wafurika kando ya vijito kusubiri chakula cha msaada

Maelfu ya raia ambao wamekumbwa na baa la njaa lililosababishwa na shughuli za binadamu nchini Sudan Kusini, wamekimbilia kwenye maeneo ya mabwawa na mito mwishoni mwa juma wakitumaini kupokea chakula cha msaada. 

Kijana wa Sudan Kusini akiwa amembeba mdogo wake wakivuka mto kuelekea eneo ambalo wataanza kupokea chakula cha msaada.
Kijana wa Sudan Kusini akiwa amembeba mdogo wake wakivuka mto kuelekea eneo ambalo wataanza kupokea chakula cha msaada. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi sasa Bol Mol mwenye umri wa miaka 45 ambaye alikuwa mlinzi wa zamani kwenye kituo cha mafuta, amekuwa akipambana kwaajili ya familia yake kuishi, akifanya shughuli za uvuvi kwenye mito ya jirani huku wake zake watatu wakitafuta maji kwaajili ya chakula.

Wanakula mlo mmoja tu ikiwa watapata bahati, lakini wanasema ni bora wakaishi kando na mito hiyo kwa usalama wao dhidi ya wanajeshi wenye silaha wanaofanya vitendo vya kihalifu.

"Maisha hapa hayana umuhimu" amesema Mol ambaye alikuwa anaonekana mchovu huku akiendelea kuwasubiri mamia ya raia wengine wanaowasili kwenye eneo hilo kwa msaada.

Mashirika ya misaada yameshauriana na Serikali ya Sudan Kusini na waasi kuanzisha vituo maalumu vya kufanya usajili tayari kwaajili ya kuanza kupokea chakula cha msaada ambacho kitaanza kupelekwa hivi karibuni.

Umoja wa Mataifa ulitangaza baa la njaa nchini Sudan Kusini wiki moja iliyopita, lakini njaa imesababisha madhara kwa zaidi ya watu wanaokadiriwa kufikia laki 1, ambapo wataalamu wanasema hali hiyo haikutokana na sababu za mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa zaidi ya miaka mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vimesabisha raia kushindwa kufanya kilimo, vimeharibu hazina za vyakula na kuwalazimisha raia kuyakimbia makazi yao.

Misafara ya misaada ya chakula na kimatibabu pia imekuwa ikishambuliwa kwa makusudi na wafanyakazi wa mashirika hayo kushambuliwa pia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.