Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Sudan Kusini haitaki tena jeshi la ukanda kulinda amani

Serikali ya Sudan Kusini inasema haitakubali tena kutumwa kwa jeshi la ukanda kulinda amani jijini Juba.

Barabara ya jiji juu la Juba nchini Sudan Kusini
Barabara ya jiji juu la Juba nchini Sudan Kusini REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Tut Gatluak mshauri ya rais Salva Kiir, ameliambia Gazeti la Sudan Tribune kuwa hakuna haja ya kutumwa kwa wanajeshi hao kutoka nchi za IGAD kwa sababu kwa sasa, hali ya usalama imeimarika.

“Usalama umeirika sana Juba, na shamrashamra za Krismasi na mwaka mpya, zilikwenda vizuri sana,” alisema Gatluk.

Gatluk ameongeza kuwa mkataba wa amani unatekelezwa ipasavyo na tayari rais Salva Kiir amezindua mazungumzo ya kitaifa, ili kuwaleta pamoja raia wa nchi hiyo.

Waziri wa Ulinzi nchini humo Kuol Manyang Juuk naye amekanusha ripoti ya kuwepo kwa mapigano mapya jijini Juba.

Akizungumza na wakaazi wa jiji hilo, Waziri huyo amewaambia kuwa ni kweli nchi yao ina changamoto nyingi lakini serikali ya rais Kiir inafanya kila iwezalo kuzitatua, na hakuna haja ya kuja kwa vikosi vya kigeni.

Aidha, amewashtumu watalaam wa Umoja wa Mataifa kwa kuandika ripoti ambazo anasema ni za uongo kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Kiongozi wa waasi Riek Machar ambaye alikuwa ni Makamu wa kwanza wa rais, alikimbia nchi hiyo mwaka uliopita, baada ya kuzuka kwa mapigano jijini Juba.

Machar kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.