Pata taarifa kuu
BURUNDI

Wakimbizi wa Burundi wajaza makambi nchini Tanzania

Kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania, zinakaribia kuzidiwa na uwezo wa kuwapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wanaoendelea kuingia nchini humo karibu kila siku.

Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini Tanzania inayowapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wa Burundi
Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini Tanzania inayowapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wa Burundi Phil Moore/Oxfam
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Kimataifa la Madktari wasiokuwa na mipaka la MSF linasema hali hii ni hatari na huenda hali ikawa mbaya zaidi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.

MSF inasema kati ya wakimbizi Laki tatu waliokimbia Burundi, zaidi ya laki mbili wanaishi nchini Tanzania katika kambi ya Nyarugusu.

Idadi hii ya wakimbizi waliofurika katika kambi hiyo inatishia kulipuka kwa magonjwa kama kipindupindu kutokana na maji safi ya kunywa, ukosefu wa chakula na hata maswala ya usalama.

00:29

Laurent Ligozat Naibu Mkurugenzi wa MSF kuhusu wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania

Akizungumza na RFI, Naibu Mkurugenzi wa MSF Laurent Ligozat amesema hali hii ikiendelea kama inavyoshuhudiwa, idadi kubwa ya wakimbizi hao hasa watoto na wanawake watakuwa katika hali mbaya ya kiafya.

“Tumeshuhudia ongezeko la wakimbizi likiongezka mara tano katika miezi ya hivi karibuni, na tunahofia hali yao ya kiafya na usalama katika siku zijazo,” ameiambia RFI.

Mama akiwa na mtoto katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu nchini Tanzania
Mama akiwa na mtoto katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu nchini Tanzania Phil Moore/Oxfam

Nalo Shirika la Kimataifa la kutoa misaada ya kibinadamu la Oxfam, katika siku za hivi karibuni limetoa onyo kama hili.

Oxfam imeendelea kuwasaidia wakimbizi hao tangu mwaka 2015 kwa kuwapa maji safi ya kunywa, chakula, mahema na kuwachimbia vyoo na maeneo ya kutupa taka.

Serikali ya Burundi katika hatua nyingine imekuwa ikisema kuwa, hali ya usalama imesharejea nchini humo na kuwataka raia wake kurudi nyumbani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.