Pata taarifa kuu
KENYA-MASHAMBULIZI

Kesi ya mashambulizi ya Chuo Kikuu cha Garissa kusikilizwa

Nchini Kenya, baada ya kuahirishwa kwa mara kadhaa, kesi ya watuhumiwa watano wa mashambulizi yaliyosababisha vifo vingi katika Chuo kikuu cha Garissa inatazamiwa kuanza Jumatatu hii katika mahakama ya mjini Nairobi.

Mwanajeshi wa Kenya katika Chuo Kikuu cha Garissa, ambapo shambulizi la kundi la Al Shebab kuotoka liliwaua watu 148, Aprili 2 mwaka 2015.
Mwanajeshi wa Kenya katika Chuo Kikuu cha Garissa, ambapo shambulizi la kundi la Al Shebab kuotoka liliwaua watu 148, Aprili 2 mwaka 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Aprili 2, 2015, kundi la wanamgambo Kiislamu wa wa Al Shebab walipenya na kuingia mapema alfajiri katika mabweni ya Chuo hicho na kuua watu 148, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 145. Washambuliaji wanne waliuawa na vikosi vya usalama, lakini vijana watano walikamatwa katika siku zilizpfuata, mshitakiwa walituhumiwa kupanga njama na wauaji.

Kwa sasa, washitakiwa hawajazungumza chochote. Raia hawa wanne kutoka Kenya wenye asili ya Somalia pamoja na raia mmoja wa Tanzania aliyebadilisha dini na kuwa Mwislamu waliharakia tu kusema kuwa hawana hatia yoyote. Kesi hii ilipofunguliwa, watuhumiwa hao walisema kuwa walifanyiwa mateso na polisi na wamekua wakiripoti mahakamani bila kujibu katika kesi hiyo.

Baadhi walikamatwa siku hiyo ya mashambulizi na wengine siku moja baadaye. Mmoja wao alikua akifanya kazi katika hoteli, wengine, walikula chakula katika hoteli hiyo siku moja kabla ya shambulio hilo. Mwengine wa pili alikuwa mlinzi katika Chuo kikuu cha Garissa, ambaye aliruhusu kundi hilo kuingia katika Chuo hicho. Alikamatwa na vikosi vya usalama wakatialipokua akituma picha za maiti nchini Somalia. Watatu, alikua na simu mbili, huku akijificha chini ya kitanda wakati askari polisi walipofika katika Chuo kikuu cha Garisa, na hakuweza kueleza kuwepo kwake katika eneo la tukio. Anatuhumiwa kuwa mmoja wa watu waliyoendesha mashambulizi kwa risasi. Na wengine wawili, ambao walitoa silaha, walikamatwa siku ya pili ndani ya basi wakati walipokua wakijaribu kuvuka mpaka.

Kesi hii ambayo imefunguliwa tangu mwaka mmoja imeendelea kuahirishwa mara kwa mara. Upande wa mashtaka, hata hivyo, unatazamia kufunga vikao vyake vya kuwasikiliza mashahidi katika wiki chache zijazo.

Je ni katika muktadha huu serikali ya Kenya ilitangaza nia yake ya kuifunga kambi ya wakimbizi wa Kisomali ya Dadaab, licha ya jumuiya ya kimataifa kupinga jambo hilo. Mkurugenzi kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani amesema shambulio la Garissa, lakini pia lile lililotokea katika jengo la kibiashara la Westgate yalipangwa katika kambi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.