Pata taarifa kuu
Habari RFI-Ki

Kenya yasema itakuwa na sheria mahsusi ya kukabiliana na wanamichezo wanaotumia dawa za kusisimua misuli

Imechapishwa:

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema nchi yake itakuwa na sheria ya kupambana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa wanamichezo hasa kwa wanariadha, kama inavyotakiwa na Shirika la Kimataifa linalopambana na dawa hizo WADA kufikia tarehe 2 mwezi Mei.

Matangazo ya kibiashara

WADA inasema ikiwa Kenya haitakuwa na sheria hii, itafungiwa kushiriki katika mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Brazil mwezi Agosti mwaka huu.

Kumekuwa na madai ya baadhi ya wanariadha wa Kenya kutumia dawa hizo na rais Kenyatta amesisitiza kuwa sheria hiyo itapitishwa Bungeni kufikia wiki ijayo na kutiwa saini.

Je sheria pekee inatosha kukabiliana na tatizo hili si tu huko nchini Kenya lakini kote duniani.

Urusi tayari imefungiwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa baada ya wanariadha wake kupatikana kutumia dawa hizo.

Vipindi vingine
  • 10:03
  • 10:06
  • 10:09
  • 10:00
  • 10:13
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.