Pata taarifa kuu

RDC: Huenda Stanis Bujakera ataachiwa kati ya leo ama siku zijazo

Nairobi – Mwanahabari mashuhuri nchini DRC, Stanis Bujakera, hapo jana alihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela pamoja na kulipa faini ya dola za Marekani 400, baada ya kukutwa na hatia ya kuvujisha taarifa kuhusu mauaji ya mwanasiasa Cherubin Okende.

Stanis Bujakera, alihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela pamoja na kulipa faini ya dola za Marekani 400.
Stanis Bujakera, alihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela pamoja na kulipa faini ya dola za Marekani 400. © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

Bujakera amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi 6 tangu alipokamatwa mwezi Septemba mwaka uliopita baada ya chapisho lake katika jarida la Jeune Afrique, ambapo alidai wanajeshi wa Serikali walihusika na mauaji ya mwanasiasa huyo.

Licha ya hukumu hii na uwezekano wa Bujakera kuachiwa kati ya leo ama siku zijazo, mawakili wake wamesema watamshauri mteja wao kukata rufaa kwa kile wanasema utetezi wao waliowasilisha mahakamani haukufanyiwa kazi na mahakama.

Tayari waajiri wake, likiwemo shirika la kimataifa la wanahabari wasio na mipaka RSF, wamekashifu hukumu hiyo, wakisisitiza kuwa tangu awali, mashtaka dhidi yake hayakupaswa kufunguliwa kwa kuwa yalichochewa kisiasa.

Hukumu hii imetolewa majuma kadhaa kupita tangu rais felix Tshisekedi, adai kuwa atalitazama upya suala la mwanahabari huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.