Pata taarifa kuu

RDC: Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde, amejiuzulu

Nairobi – Waziri mkuu wa nchi ya DRC, Jean-Michel Sama Lukonde, amejiuzulu nafasi yake hapo jana, uamuzi unaomaanisha kuvunjwa kwa Serikali yake, ikulu ya Kinshasa imethibitisha, hata hivyo bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Aliyekuwa Waziri mkuu wa nchi ya DRC, Jean-Michel Sama Lukonde
Aliyekuwa Waziri mkuu wa nchi ya DRC, Jean-Michel Sama Lukonde © RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kujiuzulu kwake inakuja baada ya Muda wa siku 8 uliokuwa umetolewa kwa wajumbe wa Serikali waliochaguliwa kuwa wabunge wa bunge la taifa nchini humo kumalizika Jumanne Februari 20 saa sita usiku.

Lukonde amechagua kushiriki vikao vya Bunge kwa mujibu wa matakwa ya Ibara ya 108 ya Katiba inayowataka viongozi waliochaguliwa kuchagua kati ya kazi zao serikalini na kuwawakilisha wananchi.

Awali, baadhi ya waliokuwa mawaziri wa timu yake nao waliwasilisha barua za kujiuzulu kwa rais miongoni mwao Vital Kamerhe (naibu Waziri Mkuu wa Uchumi), Jean-Pierre Lihau, Antipas Mbusa (Waziri anayesimamia Ushirikiano wa Kikanda) Julien Paluku kama Waziri wa Viwanda na wengine.

Sama Lukonde aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mnamo Februari 15, 2021, mwishoni mwa mashauriano ya kitaifa ambayo rais Tshisekedi aliyaanzisha Novemba 2020, hata hivyo akiwataka baadhi kusalia hadi pale atakapoteua serikali mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.