Pata taarifa kuu

ICC : Karim Khan amejiondoa katika kesi zote zinazohusiana na Kenya

Nairobi – Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC, Karim Khan, ametangza kujiondoa katika kesi zote zinazohusisha nchi ya Kenya.

Khan amechukua hatua hiyo kutokana na uhusiano wake wa awali na rais wa sasa wa Kenya, William Ruto
Khan amechukua hatua hiyo kutokana na uhusiano wake wa awali na rais wa sasa wa Kenya, William Ruto © Mary Altaffer, AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa afisi ya kiongozi wa mashtaka huko Hague, Khan amechukua hatua hiyo kutokana na uhusiano wake wa awali na rais wa sasa wa Kenya, William Ruto, ambapo khan alikuwa wakili wake katika mahakama hiyo wakati Ruto alikuwa mshtakiwa, afisi ya khana ikisema ajiondoa ili pasiwe na mgongano wa kimasilahi.

Afisi ya kiongozi wa mashatka wa ICC hata hivyo inasema sheria ya mahakama hiyo inamruhusu khana kufanya ziara za kibanafsi na kutokana hilo khana amejiondoa katika kesi zote zitakazo husisha nchi ya Kenya.

Karim Khan, kwa wakati mmoja alimwakilisha rais Ruto wakati akiwa na kesi ICC
Karim Khan, kwa wakati mmoja alimwakilisha rais Ruto wakati akiwa na kesi ICC © AP/Peter Dejong

Ni hatua inayokuja baada ya Khan kufanya ziara ya kibinafusi nchini Kenya, mwishoni mwa juma na kuhudhuria hafla ya kufunzu kwa mahafala katika chuo cha Mt Kenya, alipotuzwa kutokana na mchango wake wa kuhakikisha haki inapatikana, upinzani nchini humo ukidai ziara yake huenda ikahitilafiana na uchuguzi wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wandamanaji, katika kesi yake ambayo upinzani umewasilisha kwa ICC.

Khana amekuwa kiongozi wa mashataka katika mahakama ya ICC tangu mwaka 2021 baada ya kustaafu kwa Fatuou Bensouda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.