Pata taarifa kuu

Hoteli nne, nyumba moja zaungua moto Zanzibar

Hoteli nne na nyumba moja ya makazi zimeungua moto katika eneo la Paje katika wilaya ya kusini mwa Unguja, katika mkoa wa Kusini mwa Unguja, Zanzibar.

Mkasaba amesema wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Zimamoto wamefanikiwa kuzima moto huo bila kuleta madhara zaidi.
Mkasaba amesema wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Zimamoto wamefanikiwa kuzima moto huo bila kuleta madhara zaidi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hoteli hizo ni pamoja na Cristal Resort, Maisha Matam, Drifters na The Nest Boutique Resort, kulingana na Mkuu wa wilaya hiyo na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Rajab Mkasaba, akinukuliwa na Mwananchi Digital, huku akiongeza kuwa tukio hilo lilitokea saasaa 6:00 usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Julai 9, 2023.

"Kuna hoteli nne na ntumba moja ya kulala wageni hapa Paje zimeungua sehemu ya mapokezi kutokana na moto, baadhi ya wafanyakazi wanasema moto umeanziajikoni lakini bado uchunguzi unaendelea, " amesema Mkasaba.

Amesema hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo na kwamba moto huo umeenea kwenye hoteli zote hizo kwa sababu ya upepo na ikizingatiwa zimeezekwa kwa makuti.

Mkasaba amesema wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Zimamoto wamefanikiwa kuzima moto huo bila kuleta madhara zaidi.

Akiongea mapema leo asubuhi, Mkuu wa polisi katika mkoa huo, Gaudianus Kamugisha amethibitiha kutokea kwa ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.