Pata taarifa kuu

Burundi : Serikali yasitisha shughuli zote za chama kikuu cha upinzani CNL

NAIROBI – Wizara ya mambo ya ndani nchini Burundi imetangaza kusitisha shughuli zote za chama kikuu cha upinzani CNL, hatua ambayo wakosoaji wameitaja kama jaribio la kuzima upinzani kuelekea uchaguzi wa ubunge wa 2025.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani  cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwasa.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwasa. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika waraka wa tarehe 2 Juni, waziri analenga haswa makongamano ya chama pinzani cha Agathon Rwasa yaliyoandaliwa mwezi Machi na Aprili. Mikutano ambayo kwa mujibu wa mamlaka ilikuwa na makosa

Wizara inaamini kuwa makosa haya yamesababisha mvutano ndani ya CNL na, ili kuepusha makabiliano kati ya wanachama wa chama hicho, wizara imechagua kusimamisha shughuli zake zote hadi utekelezaji wa mfululizo wa mapendekezo.

Uongozi wa chama ulishutumu "ukiukwaji mkubwa wa Katiba" na "jaribio la kuvuruga na kudhoofisha chama cha CNL" katika nchi hii iliopo  eneo la Maziwa Makuu ambayo mara kwa mara imekuwa ikinyooshewa kidole kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Uamuzi huu unafuatia makongamano mawili - moja la kawaida mnamo Machi 12 na lengine lisilo la kawaida mnamo Aprili 30 - yanayolenga kukipa chama sheria mpya na kanuni za ndani kwa mujibu wa mgawanyiko mpya wa kiutawala wa nchi, ambao utaanza kutumika mwaka 2025.

Mikutano hii pia ilishuhudia watendaji wanane wanaompinga rais wa CNL, Agathon Rwasa, wakifukuzwa kutoka ofisi ya kisiasa.

Mwisho alikuwa amewasilisha malalamiko kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Manispaa na Usalama wa Umma, Martin Niteretse, ambaye mwishoni mwa Mei alipinga maamuzi yaliyochukuliwa wakati wa makongamano haya.

Katika barua iliyotumwa kwa Agathon Rwasa ya tarehe 2 Juni na kuwekwa hadharani siku ya Jumanne, waziri anataja "mapungufu" kuhusiana na sheria za CNL, ambazo zinatoa hasa kufanyika kwa mkutano wa ofisi ya kisiasa kabla ya kongamano lolote. "Shughuli zote zinazoandaliwa na vyombo vilivyoanzishwa kinyume na utaratibu husitishwa kote nchini", anamalizia na kubainisha kuwa "mikutano iliyoandaliwa kwa lengo la kutuliza mivutano ndani ya chama ndiyo inaruhusiwa"

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.