Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Burundi: 'Hatuegemei upande wowote' katika vita vya Ukraine

Burundi imetangaza bayana siku ya Jumanne kwamba "haiungi mkono upande wowote" katika mzozo wa Ukraine, ikisema kuwa "hakuna anayeweza kushinda vita hivi", wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov nchini humo.

Rais wa Burundi, Jenerali Evariste Ndayishmiye amepokea Jumanne hii, Mei 30, ujumbe wa Urusi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi Sergei Lavrov akizuru Burundi.
Rais wa Burundi, Jenerali Evariste Ndayishmiye amepokea Jumanne hii, Mei 30, ujumbe wa Urusi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi Sergei Lavrov akizuru Burundi. © Ntare Rushatsi House/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Februari, Burundi, nchi inayopatikana katika kanda ya Maziwa Makuu, ilijizuia kupigia kura azimio la hivi punde la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililoitaka Urusi kuondoa vikosi vyake nchini Ukraine. Jumla ya nchi 22 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa Afrika zilijizuia au hazikushiriki katika kura hiyo, na nchi mbili - Eritrea na Mali - zilipiga kura ya kupinga.

"Tumechukua msimamo wa kutojihusisha, msimamo wa kutoegemea upande wowote, wa kutofungamana na upande wowote ili kuzuia mzozo huu usifikie kanda zingine, hasa Afrika, lazima tupunguze athari za mzozo huu, (…) na huo ndio msimamo wa nchi nyingi za Kiafrika kuhusu suala hili", ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Bujumbura Albert Shingiro, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, mbele ya mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov. "Hakuna mtu anayeweza kushinda vita hivi," Bw. Shingiro pia amesema.

"Tunathamini sana msimamo wa Burundi wenye uwiano na uwajibikaji, na juu ya yote ukweli kwamba Burundi inaelewa vyema sababu za mzozo huu," amesema Sergueï Lavrov, akiongeza: "Tumezungumza pia juu ya haja ya kufanya mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ukweli kwamba Afrika haikuwa na uwakilishi wa kutosha."

Lavrov alikuwa ziarani nchini Kenya siku ya Jumatatu, ambayo inafuatia safari ya mwenzake wa Ukraine Dmytro Kouleba katika nchi kadhaa za Afrika, zikiwemo Ethiopia na Rwanda, wiki iliyopita. Moscow na Kyiv wanataka kuongeza ushawishi wao katika bara la Afrika.

Bwana Lavrov tayari ametembelea Afrika mara mbili tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine mwishoni mwa mwezi Februari 2022, wakati wa ziara yake katika nchi kadhaa. Kwa upande wake, Bw Kouleba wiki jana alitoa wito kwa baadhi ya nchi za bara hilo kukomesha msimamo wao wa "kutounga mkono upande wowote" katika vita vya Ukraine na pia alisema anataka kuimarisha uhusiano wa Kiev na bara hilo ambalo lina wakaazi bilioni 1.3, hasa kwa kutangaza ufunguzi wa balozi mpya.

Urusi ina uhusiano na nchi za Kiafrika kuanzia Vita Baridi, wakati Umoja wa Kisovieti ulijidhihirisha kuwa muangamizi wa ubeberu. Mkutano wa kilele wa Urusi naAfrika, wa pili wa aina yake, umepangwa kufanyika Julai 26-29 huko St. Petersburg (Urusi).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.