Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov anazuru Kenya

NAIROBI – Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergey Lavrov amewasili jijini Nairobi, katika ziara ambayo haikutangazwa.

Sergei Lavrov anafanya ziara nchini Kenya
Sergei Lavrov anafanya ziara nchini Kenya © MFA RUSSIA
Matangazo ya kibiashara

Ukurasa wa Twitter wa Ubalozi wa Urusi nchini Kenya, umeandika kuwa itakuwa ni wiki ya mafanikio kati ya Kenya na Urusi.

Ziara hii inakuja baada mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba kufanya ziara barani Afrika.

Inatarajiwa kuwa huenda kiongozi huyo akakutana na rais wa Kenya William Ruto amabye hajaungana na viongozi wengine wa Afrika katika hafla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu hii leo Jumatatu.

Sergey Lavrov amefanya mkutano na uongozi wa Bunge la Kenya mjini Nairobi.

Sergey Lavrov amefanya kikao na uongozi wa bunge la Kenya
Sergey Lavrov amefanya kikao na uongozi wa bunge la Kenya © MFA RUSSIA

Awali kiongozi huyo alikutana na spika wa bunge la kitaifa nchini Kenya Moses Wetangula afisini mwake.

Lavrov amekuwa akifanya ziara katika mataifa ya Afrika katika siku za hivi punde, matukio ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa huenda ni njia moja ya Urusi kutafuta mbinu za kupata ushawishi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.