Pata taarifa kuu

MSF inatoa matibabu kwa wanawake waliobakwa katika machafuko Kivu Kaskazini, DRC

NAIROBI – Nchini DRC, Madaktari kutoka Shirika la MSF kwa kipindi cha wiki mbili wamekuwa wakitoa msaada wa matibabu kwa mamia ya wanawake waliobakwa Kivu Kaskazini kutokana na utovu wa usalama, na kulazimika kuyakimbia makaazi yao.

MSF imekuwa ikitoa matibabu kwa waathiriwa wa vitendo vya ubakaji katika eneo la Kivu Kaskazini
MSF imekuwa ikitoa matibabu kwa waathiriwa wa vitendo vya ubakaji katika eneo la Kivu Kaskazini © MSF EAST AFRICA
Matangazo ya kibiashara

RFI Kiswahili imezungumza na mmoja wa akina mama walioathirika

“Nilipoenda kutafuta mkaa nilikutana na watu waliokuwa wamevalia sare za kijeshi tulikuwa wanawake watano wengine wakakimbia japokuwa mimi sikuwa na nguvu za kukimbia, nilijeruhiwa baada ya kubakwa” mmoja wa akina mama waliobakwa.

00:11

Mama aliyebakwa wakati wa machafuko Kivu Kaskazini DRC

Mama huyo ameeleza changamoto za maisha anazokabiliana nazo baada yake kubakwa.

“Baada ya kupitia changamoto hiyo niliaanza kupokea matibabu nimekuwa nikiishi maisha ya kuteseka na sina mume na nina watoto saba naomba tu serikali ya Congo ipate njia ya kumaliza vita.”alielezea Zaidi mama huyo .

00:09

Changamoto anazopitia mama huyo aliyebakwa Kivu Kaskazini

Naye Jason Rizzo, mratibu wa dharura wa madaktari wasiokuwa na mipaka huko Kivu Kaskazini amesema kwa sasa timu yao ya matibabu inawashugulikia  wahasiriwa wapya 48 wa ukatili wa kijinsia kwa siku ,kwenye kambi walizohamishiwa.

“Kwa miezi kadhaa tumeshuhudia unyanyasaji mkubwa wa kijinsia wakati tukiwa katika harakati za kutoa dawa kwa waathiriwa wa Ubakaji, tukihitaji uharaka wa kimatibabu na kibinadamu,upatikanaji wa maji na chakula kwa ajili ya walioathirika.” alisema Jason Rizzo, mratibu wa dharura wa MSF.

00:26

Jason Rizzo, Mratibu wa MSF DRC

Hayo yashuhudiwa Wakati Raia waishio kambini kandoni mwa Mji wa Goma wakabiliana piya na ugonjwa wa kipindipindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.