Pata taarifa kuu

Katibu mkuu wa UN kuhudhuria mkutano kuhusu usalama mashariki ya DRC

NAIROBI – Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, mwishoni mwa juma hili anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za ukanda mjini Bujumbura, kujadiliana kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres AP
Matangazo ya kibiashara

Guterres, atawasili nchini Burundi, akitokea nchini Kenya, ambako Jumatano ya wiki hii atakuwa na mazungumzo na rais wa Kenya, William Ruto, ambapo watajadiliana kuhusu hali ya usalama nchini Sudan na DRC.

Mbali na Sudan, akiwa nchini Kenya, pia atajadiliana na mwenyeji Wake kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa kuhusu kudhibiti usalama mashariki mwa nchi ya DRC.

Baada ya hapo, Guterres atatarajiwa nchini Burundi, ambako atakutana na rais Evariste Ndayishimiye, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo watajadiliana kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC kabla ya kushiriki kikao na viongozi wengine wa ukanda.

Ziara yake inakuja wakati huu ambapo, wakuu wa nchi wanatarajia kujadili hatua zilizochukuiliwa kuhusu mkataba wa amani wa Angola, pamoja na wajibu wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambavyo viko nchini Congo kwa miezi kadhaa sasa.

Mkutano huu wa wakuu wa nchi za maziwa makuu, utafanyika huku makundi ya waasi likiwemo lile la M23, lililotakiwa kuachia maeneo inayoyakalia mashariki mwa nchi hiyo, yakiendelea kutatiza usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela dhidi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.