Pata taarifa kuu

Kenya: Rais Ruto awataka raia kufuata sheria wakati huu maandamano yakishika kasi

NAIROBI – Nchini Kenya, kuelekea maandamano mengine ya upinzani hapo kesho rais William Ruto akizungumza akiwa nchini Ujerumani, amesema watu nchini mwake ni lazima wafuate sheria, huku akionya kuwa wale wanaohusika na uharibifu wa mali za watu, wakati wa maandamano hayo yaliyoharamishwa, watachukuliwa hatua za kisheria.

William Ruto rais wa Kenya
William Ruto rais wa Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

“Kenya ni nchi ya utawala wa sharia, tunaowajibu wa kumlinda kila mtu na polisi wanapaswa kuwa na uwezo huo.”ameeleza rais Ruto.

00:22

Rais wa Kenya William Ruto kuhusu Kenya

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, anayeongoza maandamano hayo kushinikiza kupunguzwa kwa gharama ya maisha na kutaka kufunguliwa kwa mitambo inayohifadhi matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita, amesisitiza kuwa maandamano hayo yataendelea.

Sisi tumesisitiza kwamba tutaendelea kufuata sheria.”amesisitiza Odinga.

00:07

Raila Odinga kuhusu Maandamano Kenya

Umoja wa Afrika, umetoa wito wa utulivu nchini Kenya, na kutaka serikali na upinzani kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kupata suluhu ili kumaliza vurugu zinazoendelea.

Hayo yanajiri wakati huu maofisa wa polisi katika taifa hilo la Afrika Mashariki wakiahidi kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliohusika na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya siku ya Jumatatu ya wiki hii.

Nayo Marekani imetoa tahadhari ya usalama kwa raia wake wanaoishi nchini Kenya, ikiwaonya kuhusu maandamano ya nchi nzima dhidi ya serikali ambayo yanaweza kufanyika kila wiki kwa muda usiojulikana nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.